wandishi wa habari watakiwa kuepuka kuandika habari zinazo wadhalilisha watu wenye ulemavu
NA FATMA
HAMAD PEMBA 9/3/ 2022.
Wandishiwa
habari wametakiwa kufuata miko na madili ya kazi yao wakati wanapoandika na kuripoti habari za watu wenye ulemavu ili
kulinda utu, heshima ya kundi la watu hao.
Akizungumza katika mkutano wa kuwajengea uwezo wa kuripoti
habari za watu wenye ulemavu wandishi wa
habari wa Unguja na Pemba huko hoteli ya Maru maru Juma Salum Ali kutoka Shujuwaza amesema watu wenye ulemavu
wanahaki ya kulindwa, kuheshimiwa na kuthaminiwa kama watu wengine.
‘’Niwaombe sana
epukeni kutumia majina mabaya wakati mnapoandika na kuripoti habari za
watu wenye ulemavu ambayo yanaleta
viashiria vya udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu’’ alisema Juma Salum.
Kwa upande
wake Ussi Khamis ameeleza kuwa watu
wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za
kijamii ikiwemo Ajira Elimu na kushika nafasi za uongozi, hivyo ni vyema wanahabari kupaza sauti zenu kuzisemea kero hizo hali ambayo itasaidia
kuondosha matatizo hayo.
Nao wandishi
wa habari walionufaika na mafunzo hayo wamesema kundi kubwa la watu wenye
ulemavu wenyewe bado hawazifahamu sheria
wala haki zao stahiki ambazo
wanatakiwa na wao wazipate , hivyo ni budi kwa jumuia zinazoshuhulikia watu hao
kuwapa elimu ili waweze kufuatilia wakati wanaponyimwa haki zao.
Comments
Post a Comment