WANDISHI WA HABARI PEMBA WAPIGWA MSASA
NA FATMA
HAMAD
Wandishi wa
habari wametakiwa kuielimisha jamii
kufahamu masuala ya Afya ya uzazi, ili
kufahamu afya zao, na kuweza kupata tiba
sahihi, jambo ambalo litasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Ushauri huo umetolewa na afisa mradi wa afya ya uzazi, wakati
akielezea kuhusu mradi huo wa uzazi salama Zaina Abdala Mzee kwenye mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo
wandishi wa habari, kuandika habari zinazo husu masuala ya afya ya uzazi, yaliofanyika katika ukumbi wa Tamwa Chake Chake
Pemba.
Alisema kwa mujibu wa tafiti kutoka wizara ya afya, vifo vya mama na mtoto bado ni changamoto inayoikumba Jamii.
Alisema wandishi wa habari wana nafasi kubwa katika jamii,
hivyo ni vyema kuwandika habari pamoja na makala ambazo zitaisaidia jamii
kufahamu masuala ya afya ya uzazi ili
waweze kufika vituo vya afya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu.
‘’Nyinyi waandishi wa habari mnaaminika zaidi katika jamii,
hivyo ni vyema mkayatumia mafunzo haya kwa kuielimisha jamii ili kuona lile
lengo hasa la mradi huu la kupunguza tatizo la vifo vya mama na mtoto
limefikiwa’’, alieleza afisa mradi.
Alifahamisha kuwa wameamua kuleta mpango huo ili wandishi wa
habai waweze kuielimisha jamii, ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Alisema suala la afya ya uzazi si suala la mwanamke peke yake
bali linahitajika kwa kila mtu jambo ambalo litasaidia jamii kuondokana na
maradhi.
Mapema akifungua mafunzo hayo afisa Ufuatiliaji na tathmini kutoka Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [Tamwa] Mohamed Khatib Mohamed alisema lengo la kuwapatia mafunzo hayo ni kuwasaidia wandishi wa habari kuibua changamoto zinazo wakumba wanajamii, katika upatikanaji wa huduma ili ziweze kusikika na kupatiwa ufumbuzi.
Akiwasilisha mada juu ya mazingira ya kidini na kitamaduni
kuhusu haki ya afya uzazi, Sheikh
Abdalla Nassor Abdalla kutoka
jumuia ya maimamu Zanzibar ofisi ya Pemba [ JUMAZA] alisema ni vyema kwa vijana
watakaoingia kwenye ndoa kupima afya zao kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Alifahamisha kuwa afya
ya uzazi inanzia pale kipindi cha ujauzito hadi kufikia kwenye makuzi, malezi,
na matunzo ya mtoto.
Mradi huu wa afya ya uzazi ni mashirikiano ya Tamwa Bara na
Tamwa Zanzibar chini ya ufadhili wa wellsring Phianthrepi und[WP] kutoka nchini
Marekani.
Comments
Post a Comment