ALIEMNAJISI MTOTO MWENYE ULEMAVU WA AKILI AENDELEA KUSOTA RUMANDE
Na Fatma Hamad Pemba.
Mahakama ya mkoa A wete imeighairisha kesi ya kunajisi
mtoto mwenye ulemavu wa akili inayomkabili kijana Khamis Salim Ali mwenye umri wa miaka 27 mkaazi wa Selemu wilaya ya wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
Imedaiwa mahakamani
hapo siku ya tarehe
5/2/2023 majira ya skumi
za jioni huko Selemu Wete
ulimuingialia mtoto wa Kiume
mwenye umri wa
miaka 12 ambae ni mwenye ulemavu
wa akili jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP Juma Mussa Omar
amesema kuwa kesi hiyo ilikua katika hatua ya utetezi lakini hatutoendelea
kwani hakimu anaesikiliza kesi hiyo
hayupo.
Hakimu wa
mahakama ya mkoa A Said Hemed
amesema hakimu anaendesha kesi
za udhalilishaji hayupo mahakamani amepata dharura ya kikazi nje ya Pemba kesi
hiyo itarudi tena mahakamani hapo tarehe
12/7/ 2023 na kuendelea na utetezi.
‘’Naighairisha
kesi hiyo hadi tarehe 12/ 7/ 2023 na mtuhumiwa ataendelea kukaa rumande’’
alieleza hakimu Said.
Kunajisi
mtoto mwenye ulemavu wa akili imedaiwa
ni kosa kinyume na kifungu cha [116] [1] cha sheria nambari 6/2018 sheria
ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment