WAKULIMA WA VIUNGO PEMBA WAIPA TANO MRADI WA VIUNGO.

             NA FATMA HAMAD PEMBA.

Wakulima wa  mazao  ya  Viungo    kisiwani Pemba  wameushukuru  mradi  wa  viungo  ambao  unatekelezwa  kwa  mashirikiano  ya  Tamwa Zanzibe, PDF, na CFP kwa ufadhili wa  umoja  wa Ulaya kwani  umeweza  kubadilisha  maisha  yao  na kupiga hatua  kimaendeleo.

Wakizungumza  na wandishi wa vyombo mbali mbali vya habari  kwa  nyakati  tofauti  katika ziara maalumu  iyondaliwa na Chama cha wandishi wa habari Wanawake Tanzania oisi ya Pemba wamesema mradi wa iungo umekua ni mkombozi kwao.

Asha ali Omar mkulima wa Mdalasini na vanila  kutoka Gando wilaya ya Wete  alisema  kabla ya kuja kwa mradi wa viungo  alikua  amepanda mashina 5 tu ya mdalasini, na akipanda pembeni mwa  Nyumba  yake kwani alikua hana ujuzi wa kilimo hicho.

‘’Baada  ya kuja kwa mradi wa viungo na kutupatia elimu sasa hivi nina miliki Hekari moja  ya Midalasini  na Mivanila 120  yangu  peke yangu alisema mkulima bi Asha.

Alisema kilimo hicho kimekua kikimpatia tija kwani ameweza kusomeshea Watoto wake, kujenga nyumba ya mtoto wake  pamoja na kuendeshea shughuli zake za kimaisha.

‘’Kwa kweli kabla sijapata elimu hii ya ukulima wa Midalasini na Mivanila hali yangu ilikua ngumu kiasi ambacho  nilikua nashindwa kuihudumia familia yangu’’ alieleza bi Asha.

Kwa upande wake Subira Mkubwa pamoja Mohd Khamis wakulima wa kilimo cha Mananasi, Mapensheni na Pili pili boga kutoka Kwale mpona walisema kabla ya kuja kwa mradi wa viungo walikua wakilima kilimo cha Mihogo tu, na ilikua haiwaletei faida kubwa.

‘’Tunaushukuru mradi wa viungo kutupatia taaluma  kwani  kwa sasa tumekua tukizalisha mazo mengi  kwa wingi  jambo ambalo limetuanya tupige hatua kimaendeleo.

Aidha wakitaja  faida wanazozipata kupitia kilimo chao wamenunua Vespa, wametia umeme  Nyumbani  mwao,  wameanzisha fondesheni ya nyumba samba mba na kuendeshea mahisha yao.

Mapema mkulima  wa mboga mboga  kutoka Vitongoji  Chake chake Mkunga Hamad Sdala  alisema kabla hajapata  mafunzo  kutoka  kwa mradi wa Viungo alianzisha  kilimo  kwa  mtaji  wa  shilingi  Milioni  moja  kwani  alikua akilima  Pili  pili na  mboga  za  majani tu.

‘’Mradi wa viungo umeninufaisha pakubwa kwani baada ya kupata ujuzi nimeongeza ukulima wa Mahindi, Migomba ambapo nimefikia mtaji zaidi ya Milioni moja’’Alifahamisha bi Mkunga.

Aliendelea kufahamisha kuwa licha ya hayo  pia  alinunua mbuzi 2 baada  ya  kuuza  mazao  aliyoyazalisha  shambani  kwake.

Omar Salum Mbarouk nae mkulima wa mboga mboga wa Vitongoji aliwataka Vijana wenzake kujikita katika sekta ya kilimo ili waweze kujipatia ajira.

‘’Mimi nilikua dereva wa gari aina ya keri ila niliwacha ilikuwa hainilipi, lakini  baada ya kujingiza kwenye kilimo kwa muda wa miezi Minne tu nilipata faida na sasahivi najenga Nyumba’’ alisema Mkulima Salum.

Nae Afisa kutoka mradi wa Viungo Pemba  Hadhir  Ilibasi Sezero alisema kutokana na elimu  ambayo  wanawapatia  wakulima kumesaidia kwa kiasi kikubwa kwani wamekuwa wakiongeza uzalishaji  jambo ambalo litawawezesha kutatua changamoto za maisha yao.

‘’Kwa mwezi uliopita kuna wakulima tuliwapatia Miche 500, 400, hadi 100 ya Midalasini na Mivanila  kwa mtu mmoja  ambapo  zamani ilikua wakipanda miche Hamsini tu, kwani walikuwa hawana elimu ya  kilimo hicho’’  alisema Afisa.

Alisema wamekuwa wakiwaunganisha wakulima wao na Masoko ya ndani na nje ili kuona wanauza ili kuona wanauza mazao yao samba na kujipatia kipato.ndishi wa vyombo mbali mbali vya habari  kwa  nyakati  tofauti  katika ziara maalumu  iyondaliwa na Chama cha wandishi wa habari Wanawake Tanzania oisi ya Pemba wamesema mradi wa viungo umekua ni mkombozi kwao.

Asha ali Omar mkulima wa Mdalasini na vanila  kutoka Gando wilaya ya Wete  alisema  kabla ya kuja kwa mradi wa viungo  alikua  amepanda mashina 5 tu ya mdalasini, na akipanda pembeni mwa  Nyumba  yake kwani alikua hana ujuzi wa kilimo hicho.

‘’Baada  ya kuja kwa mradi wa viungo na kutupatia elimu sasa hivi nina miliki Hekari moja  ya Midalasini  na Mivanila 120  yangu  peke yangu alisema mkulima bi Asha.

Alisema kilimo hicho kimekua kikimpatia tija kwani ameweza kusomeshea Watoto wake, kujenga nyumba ya mtoto wake  pamoja na kuendeshea shughuli zake za kimaisha.

‘’Kwa kweli kabla sijapata elimu hii ya ukulima wa Midalasini na Mivanila hali yangu ilikua ngumu kiasi ambacho  nilikua nashindwa kuihudumia familia yangu’’ alieleza bi Asha.

Kwa upande wake Subira Mkubwa pamoja  na mume wake Ali Khamis Abdala    wakulima wa kilimo cha Mananasi, Mapensheni na Pili pili boga kutoka Kwale mpona walisema kabla ya kuja kwa mradi wa viungo walikua wakilima kilimo cha Mihogo tu, na ilikua haiwaletei faida kubwa.

‘’Tunaushukuru mradi wa viungo kutupatia taaluma  kwani  kwa sasa tumekua tukizalisha mazo mengi  kwa wingi  jambo ambalo limetuanya tupige hatua kimaendeleo.

Aidha wakitaja  faida wanazozipata kupitia kilimo chao wamenunua Vespa, wametia umeme  Nyumbani  mwao,  wameanzisha fondesheni ya nyumba samba mba na kuendeshea mahisha yao.

Mapema mkulima  wa mboga mboga  kutoka Vitongoji  Chake chake Mkunga Hamad Sdala  alisema kabla hajapata  mafunzo  kutoka  kwa mradi wa Viungo alianzisha  kilimo  kwa  mtaji  wa  shilingi  Milioni  moja  kwani  alikua akilima  Pili  pili na  mboga  za  majani tu.

‘’Mradi wa viungo umeninufaisha pakubwa kwani baada ya kupata ujuzi nimeongeza ukulima wa Mahindi, Migomba ambapo nimefikia mtaji zaidi ya Milioni moja’’Alifahamisha bi Mkunga.

Aliendelea kufahamisha kuwa licha ya hayo  pia  alinunua mbuzi 2 baada  ya  kuuza  mazao  aliyoyazalisha  shambani  kwake.

Omar Salum Mbarouk nae mkulima wa mboga mboga wa Vitongoji aliwataka Vijana wenzake kujikita katika sekta ya kilimo ili waweze kujipatia ajira.
‘’Mimi nilikua dereva wa gari aina ya keri ila niliwacha ilikuwa hainilipi, lakini  baada ya kujingiza kwenye kilimo kwa muda wa miezi Minne tu nilipata faida na sasahivi najenga Nyumba’’ alisema Mkulima Salum.

Nae Afisa kutoka mradi wa Viungo Pemba  Hadhir  Ilibasi Sezero alisema kutokana na elimu  ambayo  wanawapatia  wakulima kumesaidia kwa kiasi kikubwa kwani wamekuwa wakiongeza uzalishaji  jambo ambalo litawawezesha kutatua changamoto za maisha yao.

‘’Kwa mwezi uliopita kuna wakulima tuliwapatia Miche 500, 400, hadi 100 ya Midalasini na Mivanila  kwa mtu mmoja  ambapo  zamani ilikua wakipanda miche Hamsini tu, kwani walikuwa hawana elimu ya  kilimo hicho’’  alisema Afisa.

Alisema wamekuwa wakiwaunganisha wakulima wao na Masoko ya ndani na nje ili kuona wanauza ili kuona wanauza mazao yao samba na kujipatia kipato.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.