JAMII YAPEWA ONYO
NA FATMA HAMAD PEMBA
Jamii imehimizwa kuendelea kuziripoti katika vyombo
vya sharia kesi za udhalilishaji, na
sio kuzikalia kitako na kuzifanyia
suluhu kifemilia.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi Hakimu wa mahakama maalum ya kupambana na udhalilishaji iliyopo
Wete mkoa wa Kaskazini Pemba, Ali Abdul Rahman
Ali amesema Serilaki imefanya jitihada mbali mbali ikiwemo kuanzisha mahakama
maalum ili kuondosha tatizo hilo Nchini.
Alisema licha ya elimu
inayoendelea kutolewa kila siku kwa wanajamii, ili kufahamu madhara ya udhalilishaji, lakini
bado jamii imegubikwa na wimbi la rushwa muhali na badalayake
kuzifumbia macho na kuzifanyia suluhu wenyewe kwa wenyewe, hali ambayo
inapelekea kuongezeka kwa udhalilishaji.
‘’Ndugu wanajamii, tusipokuwa
makini na tukiendelea kumuonea huruma mdhalilishaji, bado tutaendelea kuutilia
mbolea udhalilishajikatika jamii zetu,’’ alieleza hakimu.
Hakimu huyo aliendelea
kufahamisha kuwa zipo baadhi ya familia huziripoti kesi zao, lakini mwisho wa
siku hawajitokezi mahakamani na kutoa ushahidi, na badala yake kubakia kuitupia
lawama mahakama.
‘’Mtaendelea kutulaumu kila
siku mahakimu tunakula rushwa, tunapewa hongo, lakini bila ya kuepo na ushahidi
hatuwezi kumtia mtu hatiani,’aliesema hakimu Ali.
Akitoa ushuhuda mmoja wa wahanga
wa tukio la udhalilishaji kutoka wilaya ya Micheweni, alisema baada ya mtoto
wake kudhalilishwa na kuenda kwenye vyombo vya sharia, baadhi wanafamilia
walimtenga na kumuekea vikao ili
waimalize kimya kimya, kwani mfanyaji alikua ni ndugu wa familia , hivyo atasababisha
ugonvi.
‘’ Sikujali maneno ya watu,
wala sikukubali kuimalizia mtaani,
niliendelea kuifuatilia kesi yangu na
mwisho wa siku mtuhumiwa kafungwa jela miaka 7,’’ alisema muhanga wa
udhalilishaji
Nao baadhi ya wananchi kutoka
mkoa wa kaskazini Pemba walivitaka vyombo vinavyotoa haki, kufanya kazi zao kwa uwadilifu ili kuona kila
mmoja anapata haki yake, na sio kuwangalia wenye vipato vya juu tu.
‘’Mahakama maalum imewekwa
iwe mkombozi kwa watu wote, hivyo tunawaomba mnaosimamia hizi kesi kutenda
haki, ili wanyonge nawao tupate haki zetu pindi tunapofikwa na kadhya za
udhalilisha,’’ walisema wananchi.
Jumla ya kesi 134 za
udhalilishaji zimeripotiwa katika mahakama maalum ya kupambana na udhalilishaji
mkoa wa Kaskazini Pemba, kuanzia mwaka 2021 hadi June 2023, ambapo 2021
kuliripotiwa kesi 55, 2022 63, na January hadi June 20233 kesi 15.
Comments
Post a Comment