WANACHI WAHIMIZWA KUYATUNZA NA KUYAENZI MAZINGIRA YA BAHARI
NA FATMA HAMAD, PEMBA
SERIKALI ya Mapinduzi
ya Zanzibar,imesema itahakikisha inachukua hatua za makusudi za kudhibiti uharibifu wa
mazingiara ya baharini na kuwajengea uwelewa Wananchi juu ya umuhimu wa
utunzaji wa mazingira ya baharini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi mawasiliano
na Uchukuzi Dokta Khalid Salim Mohd wakati akifunga maadhimisho ya siku ya
usafirishaji na usalama wa bahari huko Gmbani Chake chake Pemba.
Alisema binaadamu na viumbe baharini
wanategemea bahari katika maisha yao ya kila siku hivyo ni wajibu wa wanachi
kulipa umuhimu sualal la utunzaji wa mazingira ya bahari ili kulinda maisha ya
viumbe wananchi baharini.
Alisema pamoja na umuhimu huo bado
bahari inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira ikiwemo
ukataji wa mikoko, utupaji taka ovyo baharini jambo ambalo husababaisha
kupoteza maisha ya viumbe baharini pamoja na upandaji wa kina cha maji ya
bahari.
Alisema asilimia 70 ya wananchi wa Visiwa vya Zanzibar,wanategea
uchumi wa bahari kama vile shughuli za uvuvi wa samaki na ukulima wa zao la
Mwani lakini bado jamii haijakuwa na muamko juu ya athari za Mazingira ambazo
zinaweza kujitokeza.
‘’Kuna haja kwa Serikali kuwa na Mkakati
maalumu katika kudhibiti uharibifu wa mazingira kutokana na baadhi ya wananchi
kutotambua athari za mazingira wamekuwa wakitupa machupa ya pastiki na kukata
miti ovyo jambo linaloweza kuleta madhara makubwa katika nchi’’alisema
Dk,Khalid.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatibu amesifu juhudi zinzochukuliwa na Wizara ya Ujenzi mawasilino na usafirishaji kwa kuimarisha huduma za usafiri baharini na Nchi kavu.
Alisema kwa sasa inaonekana Wizara hiyo maeneo
mengi ya Pemba,ikiwa katika harakati za ujenzi wa bara bara pamoja na ujenzi wa
bandari ya Shumba jambo linatakaloweza kukuza uchumi wa nchi kutokana na
kuongezeka kwa shughuli za kibiashara baada ya kukamilika miundombinu hiyo.
Kwa upande wake Afisa uhusiano kutoka Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji Tanzania (NiT) Juma Manday alisema kuwepo kwa maonyesho hayo kunatoa fursa kwa wananchi kufahamu fursa za ajira katika fani mbali mbali zinazohusiana na bahari ikiwemo ufundi na ukarabati wa vyombo vya usafiri baharini.
Alisema Serikali ya Awamu wa sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,imelekeza nguvu zake miradi ya kimkati katika maswala ya bahari ikiwemo katika utanuzi wa bandari ambapo kuna fusa nyingi hasa kwa Vijana wanaozungukwa na maeneo ya bahari kutokana nakuwepo kwa dhana ya uchumi wa bluu hivyo Vijana kama wataweza kupata mafunzo ya fani hizo wataweza kufika mbali.
Comments
Post a Comment