MTUHUMIWA WA KESI YA ULAWITI AOMBA AACHILIWE HURU
NA FATMA HAMAD, PEMBA
MTUHUMIWA wa kesi ya kunajisi mtoto wa
kiume mwenye umri wa miaka 12, ambae ni mwenye ulemavu wa akili anaetambulika
kwa jina la Khamis Salum Ali mkaazi wa
Selemu Wete [27], ameiomba mahakama ifute kesi hiyo, kwani si ya ukeli ni ya uongo,[kusingiziwa].
Mtuhumiwa
huyo ameiomba mahakama hiyo mbele ya hakimu wa Mahakama ya kupambana na makosa
ya udhalilishaji iliyopo Wete mkoa wa kaskazini Pemba Ali Abdulrahman Ali alisema
kuwa siku hiyo aliyosingiziwa kuwa amefanya tukio hilo hakuwepo maeneyo hayo,
bali alikuwepo Chasasa kwenye shughuli zake za ujenzi.
‘ ’Mheshimiwa
Hakimu mimi sjafanya tukio hilo hizo ni njama tu zilizopangwa na wazazi na
wanakijiji wanibambikizie kesi ili ningie hatiani,’’alieleza.
Alisema kuwa
ushahidi uliotolewa na Madaktari pamoja na Askari wote ni wa uongo, hivyo
ameiomba mahakama ifute kesi hiyo na imuachie huru, kwani hajafanya tukio hilo.
Hakimu Ali Abdul rahman Ali hakukubaliana na ombi la
mtuhumiwa huyo, hivyo alimtaka arudi tena rumande hadi tarehe 21 mwezi huu kwa
ajili ya hukumu.
Imedaiwa
mahakamani hapo mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe 5/2/ 2023 majira ya
saa 10.00 za jioni huko Selemu wilaya ya Wete mkowa wa Kaskazini Pemba
alimuingilia mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12, mwenye ulemavu wa akili,
jambo ambalo ni kosa kisheria, kinyume na kifungu cha 116[1] cha sharia nambari
6/2018, sharia ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment