WANANCHI WAKERWA NA MIUNDO MBINU MIBOVU HOSPITALINI



NA FATMA HAMAD,PEMBA.

WANANCHI  wa  kijiji cha Mtangani  wanaoishi  karibu  na  kituo  cha  afya  cha  Bagamoyo  wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba wanalalamikia  juu ya kukosekana kwa  eneo malumu  la kuchomea taka  za Hospitalini hapo, jambo ambalo linaweza kupelekea kutokea kwa maradhi hatarishi ya mripuko ikiwemo kuharisha.

 Akizungumza na wandishi wa habari huko kijijini kwao  Nasra Ali Makame amesema kukosekana kwa eneo [shimo] malumu la kuchomea  taka katika kituo hicho kinawathiri, kwani wakati wa kuchomwa taka  moshi husambaa kwenye makaazi yao na kusababisha kukohoa na kupata  muamsho katika miili yao.

‘’Wanapochoma moto taka zao, moshi na harufu  yote inaingia humu ndani mwangu, Napata muwasho mimi na watoto wangu,’’alieleza.

 Said Bakari Makame alisema kuwa watoto wote  wanachejeza karibu na shimo hilo, kwani hakuna uzio katika kituo hicho.

 Alieleza kuwa kuna hatari kubwa ya waoto wanaoishi katika eneyo hilo kupata maradhi hatarishi ya mripuko, kwani  wamekuwa wakiokota vifaa viliyokwisha tumika kama vile Sindano, Glavu,pamoja na vifaa vya kupimia ujauzito, kwa ajili ya kuchezea.


 ‘’Taka zinatupwa tu ovyo ovyo, watoto wetu wanaokota na kwenda kuchezea, na wengine wanatia mdomoni kabisa, hawajui wao jee hiyo si hatari,’’alifahamisha.

Faidh khamis  Darusi  alisema ni vyema wizara ya afya kuchukua jitihada za makusudi kuboresha miundombinu ya kuhifadhia taka kituoni hapo,ili kulinda usalama wa afya kwa watoto.

‘’Watoto na wanawake ndio wathirika zaid, hivyo ipo haja kwa Serikali kufanya maboresho ya kuweka eneyo malumu kwa ajili ya kuchomea taka, bila ya kuleta athiri kwa wananchi,’’alieleza.

 Akitaja changomoto inayowakwaza katika Hospitali yao Mkuu wa kituo cha afya Bwagamoyo Asha Juma Khamis alieleza kuwa ni kukosekana kwa  eneo malumu la kuchomea taka licha ya kupeleka taarifa sehemu husika lakini bado changamoto hiyo haijatatul.

 Afisa mdhamini wizara ya afya Khamis Bilali Ali amekiri kuwepo kwa tatizo hilo kituoni hapo.

 Alifahamisha kuwa serikali kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia watoto duniani [UNICEF] wameshanza ujenzi wa tanuri katika eneyo la kwareni Vitongoji kwa ajili ya kuchomea taka kutoka Hospitali zote za Pemba, ili kuepusha uchafuzi wa mazingira ambao unasababishwa na uchomaji wa taka kiholela.

 SERA NA SHERIA.

Sera ya wizara ya Afya ya Zanzibar ya mwaka 1990 ni kuhakikisha inaimarisha huduma za afya ya uzazi ya mama na mtoto, ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na vya watoto wachanga.

 BAJETI YA SERIKALI 2023-2024.

Katika kipindi cha utekelezaji july 2022 hadi kufikia march 2023, wizara kupitia idara ya uendeshaji na utumishi inajukumu la kuhakikisha kuwa wizara inanyenzo ikiwa ni pamoja na rasili mali watu, fedha, majengo, usafiri na vitendea kazi.



Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.