PACSO YATAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA UTETEZI WA SERA, SHERIA ZINAZO MKANDAMIZA MWANAMKE.
ASASI za kirai zimetakiwa kuzisemea
na kuzifanyia utetezi Sera na Sheria ambazo zina mkandamiza mwanamke na mtoto wa kike wasifikie kwenye
malengo yao, ikiwemo kwenye ngazi za mamuzi.
Akiwasilisha
mada mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka [Zalho] Pemba Siti Habibu Muhamed
katika mkutano wa kuibua changamoto za kisera, sharia na kanuni zinazokwaza
maendeleo ya wanawake kwa asasi za kutetea haki za wanawake huko Maktaba Chake
chake Pemba.
Mwanaharakati
huyo alisema vipo vifungu kadhaa vya sharia vimekua vikimkandamiza mwanamke kushiriki
katika sekta mbali mbali, hivyo ni vyema kusimama kidete kuleta ushawishi na
utetezi, ili kuona zinafanyiwa marekebisho na mwanamke nayeye aweze
kushika nyadhifa za uongozi.
‘’Kama sisi
ni wadau wa kutetea haki za wanawake, ni budi tushirikiane kwa kuzifanyia
utetezi, ziweze kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha hazimkandamizi mwanamke
na mtoto wa kike,’’ameeleza.
Alisema
miongoni mwa vifungu hivyo ni kifungu cha 67 [1] cha katiba ya Zanzibar
kimeleza kuwa kutakuwa na wajumbe wa baraza la wawakilishi wanawake kwa idadi
ya asilimia 40 ya wajumbe wote wa kuchaguliwa kwenye majimbo ya uchaguzi.
Alifahamisha
kuwa hadi sasa ni asilimia 38 tu kwenye wajumbe hao wanawake, hivyo ipo haja
kwa wanaharakati kulisemea na kufanyiwa marekebisho, ili kufikia lengo la
asilimia hamsini kwa hamsini ya wanawake
kwenye uongozi.
Alisema
sheria nyengine ni sheria ya elimu ya mwaka 1982, adhabu zinazotolewa kwa watoto wanaofungishwa
ndoa ni ndogo,mzazi anatakiwa alipe faini isiyozidi shilingi elfu 10, na
atakaposhindwa ni kifungo cha miezi 3.
‘’Tusipoipigia
kelele sisi kama wadau tutaendelea kukosa viongozi wanawake maisha yote kwenye tasisi zetu,’’ameleza.
Pia sheria
ya Kadhi namba 9 ya mwaka 2017, haijangalia madhara yanayoyapatikana kutokana
na kukosa mtetezi [Asesa] mwanamke kwenye mahakama hiyo.
Kwa upande
wake mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na watoto wilaya ya Wete Sabah Mussa
Said alisema utetezi na uchechemuzi wa sera unahitajika kihali na mali, kwani bado
kuna watoto wenye ulemavu wamekuwa wakikosa haki zao za elimu kutokana na
kukosa miundombinu rafiki maskulini, kama vile walimu mjumuishi.
‘’Licha ya
kuwa Sera na Sheria ya elimu ya mwaka
1982, imeweka mikakati kuhakikisha watoto wote wanapata elimu, lakini bado
watoto wetu wenye ulemavu hawafaidiki na haki yao hiyo,’’alifahamisha.
Alieleza
kuwa Skuli nyingi hazina walimu wa lugha za alama kulingana na mahitaji ya mwanafunzi,
hivyo ni vyema wadau na Serikali kuliona hilo, na kuweka mazingira rafiki yatakayo
wafanya nawao kuwa viongozi bora wa badae.
‘’Mimi
mwenyewe Shuleni kwangu nilikua ninae mwenye ulemavu wa uziwi na mdomo, ila
hakukuwa na mwalimu hata mmoja aliekua akimuelewa, tulimchukua tu ilimradi
amalize tu, lakini hana alichotokanacho zaidi ya kufeli,’’alifahamisha.
Nae
mkurugenzi mtendaji wa shirika la mtandao wa asasi za kiraia Pemba [Pacso]
Muhamed Najim alisema lengo la mafunzo hayo kwa jumuiya hizo zinazotetea haki
za wanawake, ni kujadili Sera, Sheria na kanuni ambazo zinawakwaza wanawake
wasifikie malengo yao ili ziweze kujulikana na kufanyiwa marekebisho.
Pia kifungu cha 12 [ 1] kinaeleza watu wote ni sawa mbele ya sharia, na wanayo haki, bila ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sharia.
Comments
Post a Comment