WASAIDIZI WA SHERIA WAHIMIZWA KUJITUMA KWA BIDII.
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Jumuiya za wasaidizi wa sharia zimetakiwa kuanzisha miradi mbali mbali ya kimaendeleo ambayo itawapatia fursa zitakazowasaidia kupata maslahi katika jumuia zao.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kutoka jumuia ya wasaidizi wa sheria wa wilaya ya micheweni Moh’d Hassan Ali huko ofisi za wasaidizi wa sharia iliyopo Wingwi Mapofu kaskazini Pemba.
Amesema jumuiya ya wasaidizi wa sharia sio jumuia inayotengeneza kipato, lakini ni budi kuwepo na miradi ambayo itasaidia kufikia lengo la utoaji wa msaada wa kisheria kwa jamii bila ya kutegemea ufadhili.
‘’Wasaidizi wa sheria mnajukumu la kuwasaidia wananchi wakati wanapopata matatizo hivyo msikae tu mkategemea ufadhi bali na nyinyi jiongezeni ili muweze kuifikia jamii kila pembe’ alieleza mwenyekiti wa bodi.
Aidha amewataka wasaidi wa sharia kufanya kazi na vikundi vya wajasiamali pamoja na wafanya biashara ili kuhakikisha nawao wanazifahamu sharia na katiba za Nchi.
‘Wapo watu wameanzisha vikundi lakini havina usajili wala katiba, hivyo ni wajibu wenu kuwafikia na kuwaelimisha jinsi ya kuviendesha vikundi hivyo’ alishauri mwenyekiti.
Mapema msaidizi wa sharia kutoka shehia ya Tumbe magharibi Zaina Omar Othman amesema bado jamii inakabiliwa na migogoro na matatizo kadha hivyo ni wakati wasaidizi wa shria kujitoa kihali na mali kuisaidia jamii ili kuinusuru migogoro isitokezee.Nae kaimu mkurugenzi wa jumuia hiyo Saleh Hamad Juma ameeleza kuwa kuwepo na mashirkiano ya pamoja kwa jumuia za wasaidizi wa sharia ni njia pekee itakayozifanya jumuia hizo kufikia lengo lao la usaidizi wa kisheria.
Comments
Post a Comment