WADAU WAOMBA SHERIA ZINAZOHUSU MASUALA YA UDHALILISHAJI ZIFANYIWE MAREKEBISHO
NA FATMA HAMAD
PEMBA.
Mratibu wa
chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa ofisi ya Pemba Fathiya
Mussa Said amewataka wandishi wa habari kupaza sauti zao kwa kuzisemea sheria mbali mbali zenye mapungufu ambazo
zinazohusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ziweze kufanyiwa marekebisho ili zinaendana na
hali ya sasa.
Mratibu huyo
ameyasema hayo huko ofisini kwake
Mkanjuni Chake chake wakati akifunga mafunzo ya siku mbili yanayohusu
mradi wa kuhamasisha hatua za kitaifa dhidi ya vitendo vya udhalilishaji
Zanzibar kwa wandishi wa vyombo mbali mbali kisiwani Pemba .
Amesema licha
juhudi mbali mbali zinazochukuliwa ili kuondosha udhalilishaji lakini bado kuna
vifungu vya sheria vinaleta ukakasi jambo ambalo linakwaza harakati za utetezi dhidi ya masuala hayo.
‘’Vipo
vifungu mbali mbali vya sheria vinakandamiza
masuala ya udhalilishaji hivyo ni jukumu lenu wandishi wa habari kuvipiga
kelele ili kuona vinarekebishwa na kuona vinaleta mabadiliko juu ya masuala haya
ya udhalilishaji’’ alieleza mratib.
Akiwasilisha
mada mwanasheria kutoka Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka [dpp] Ali Amour Makame amesema
miongoni mwa sheria ambazo zinavifungu
vinavyoonesha mapungufu ni Sheria ya kumlinda mwari na mtoto wa mzazi mmoja,
Sheria ya Ushahidi, Sheria ya mtoto, Sheria ya Jinai na Madai.
Amesema ni
vyema vikangaliwa na kufanyiwa marekebisho vifungu vinavyoonyesha
mapungufu katika sheria hizo jambo
ambalo litaepusha migongano katika uendeshaji wa kesi hizo.
Wakiwa
katika mjadala wa pamoja wandishi waliopewa mafunzo hayo wamesema nivyema
kuwepo na adhabu kali kwa pande zote mbili mke na mume wakati watakapokutwa
wakifanya vitendo vya udhalilisha jambo ambalo litasaidia kupungua kwa matendo
hayo.
Comments
Post a Comment