WASAIDIZI WA SHERIA WAWAPIGA MSASA WAZAZI
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Jamii imekumbushwa kuacha tabia ya kuwaficha wahalifu
wanaofanya vitendo vya udhalilishaji katika familia zao jambo ambalo
linachangia kuongezeka kwa vitendo hivyo.
Ukumbusho huo umetolewa na msaidizi wa sharia kutoka jumuia
ya wasaidizi wa sharia ya wilaya ya Micheweni Salim Hemed Salim wakati
akizungumza na wananchi wa shehia ya Shumba vyamboni iliyopo wilaya ya
Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake
na watoto bado vinaendelea kufanyika, hivyo ni wakati wanajamii kuvunja ukimya
na kuwafikisha kwenye vyombo vya sharia wahalifu wanatenda makossa haya ili
kutiwa hatiani.
‘’Niwambie wazazi wenzangu kama tutaendelea kuwaficha na
kuona muhali tutawafanya watoto waendelee kukumbwa na kadhya hiyo’’ alisema
msaidizi wa sharia.
Mapema msaidizi wa sharia kutoka shehiya ya Shumba vyamboni
Said Masoud Rashid amesema ni vyema wazazi na walezi kukaapamoja na kurudisha
malezi ya pamoja katika kuwalea watoto jambo ambalo litasaidia kuondosha
ushalilishaji.
Comments
Post a Comment