WANDISHI WATAKIWA KUZISEMEA KERO ZINAZOKATISHA NDOTO ZA WANAWAKE, WATU WENYE ULEMAVU NA VIJANA
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Wandishi wa habari wametakiwa kuibua na kuzisemea kero zinazo wakabili Wanawake, Vijana pamoja na watu wenye ulemavu ambazo zinapelekea kuwakosesha fursa mbali mbali za kimaendeleo.
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi wa hama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa
wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa njia ya mtandao kwa wandishi wa
habari wa vyombo mbali mbali kisiwani Pembakatika mafunzo ya mradi wa
kuhamasisha hatua za kitaifa dhidi ya vitendo vya udhalilishaji Zanzibar .
Amesema
Wandishi wa habari wanamchango mkubwa katika kuisaidia jamii kupiga hatua
kimaendeleo.
Hivyo
amesema kuwa wakati umefika kwa wandishi wa habari kuzisemea kero zinazo kosesha kupata haki pamoja na fursa
mbali mbali ikiwemo ya uongozi.
‘’Wandishi
wa habari endeleeni kupaza sauti kwa kuzitetea hangamoto zinazowakumba
wanawake, watu wenye ulemavu, Vijana ili kuona nawao wanaingia katika ngazi za
maamuzi’’ alisema Bi mzuri.
Akiwasilisha
mada juu ya ushiriki na ushirikishwaji wa wanawake mkufunzi wa mafunzo hayo
Sabah Mussa Said watu wenye ulemavu ni kundi ambalo maranyingi linacahwa nyuma hivyo ni vyema
wandishi mkaelekeza nguvu zenu kuuelimisha umma kufahamu kwamba watu wenye
ulemavu wanastahiki kupata mahitaji na fursa kama watu wengine.
Kwa upande
wake mratibu wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa ofisi ya
Pemba Fathiya Mussa Said amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajenga na
kuwakumbusha wandishi wa habari waweze kuandika matatizo yalioyopo kwenye jamii
ambayo yanawakumba wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwemo usawa wa
kijinsia, fursa za ushiriki na ushirikishwaji katika nafasi za uongozi, pamoja
na sheria ambazo zinamapungufu katika maswala ya udhalilishaji.
‘’Makundi
haya matatu nayo yana haki sawa kama yalivyo mengine hivyo ni wajibu wenu wandishi
wa habari kwenda kuangalia ni tatizo gani linalo fanya wasifikie ndoto
zao’’alieleza mratib Tamwa.
Nao baadhi
ya wandishi waliopata mafunzo hayo wamesema wakati umefika kwa wandishi wa habari kuielimisha jamii kuondosha zile itikadi
potofu kwamba makundi hayo hayawezi kufanya jambo lolote lenye kuleta
mabadiliko.
Mradi huo wa
miaka miwili unafadhiliwa na foundation for civil society ambao unaendeshwa na
Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [TAMWA], Zafela,Tujipe na
Kuhawa.
Comments
Post a Comment