Kamati ya Madili ya Baraza la Habari Tanzania-MCT-imesema ni marufuku kwa mujibu wa sheria ,Mandishi wa habari kuvaa sare za cha siasa .
Kamati ya
Madili ya Baraza la Habari Tanzania-MCT-imesema ni marufuku kwa mujibu wa
sheria ,Mandishi wa habari kuvaa sare za chama cha siasa wakati anapotekeleza majukumu yake hasa
katika kipindi hichi cha kampeni za uchaguzi.
Hayo yamesemwa na Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Kajub Mkajanga katika Mkutano wa Wandishi wa Habari na Vyanzo vya habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kiwanja wa michezo GombanChake chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema sio
jambo zuri kwa Mwandishi wa habari kuvaa
sare za chama kwani inaweza kuhatarisha usalama wake na vyombo vyake pamoja na
kituo anachokifanyia kazi.
‘’Kwa mujibu
wa sheria ya tume ya uchaguzi ni kosa kisheria mwandishi kuvaa sare ya chama,
hili pia hata sisi MCT tunapiga marufuku hivyo hakikisheni mnajiepusha na vitewndo
hivyo”alisisitiza.
Aidha amesema
mtu yoyote atakae mlazimisha
mwandishi kuvaa nguo ya chama atakuwa
amevunja Sheria na kanuni za uandishi wa
habari.
Amefahamisha
kuwa wandishi endapo watavaa nguo za chama wakati wa napokua
katika shuhuli zao za kihabari watambue kwamba wanahatarisha maisha yao.
Mapema makamo
mwenyekiti wa kamati ya maadili kutoka baraza la Habari Tanzania [MCT] Eda Sanga amewataka wandishi wa habari
kuandika habari zao kwa kufuata Kanuni na Misingi ya kihabari.
Wakitaja changa moto ambazozinawakabili baadhi ya wandishi walioshiriki mkutano huo wamesema ni kukosa mashirikiano
mazuri kwa baadhi ya Tasisi wakati
wanapokwenda kupata habari
Samba mba na
hayo wamelitaka Baraza la Habari MCT
kuwapa taaluma Viongozi wa Tasisi mbali mbali zikiwemo za Serikali na Binafsi
ili kufahamu umuhimu na mchango wa Wandishi wa habari.
Comments
Post a Comment