SERIKALI YATAKIWA KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA WALE WOTE WANAOZIFANYIA SULUHU KESI UDHALILISHAJI
NA FATMA HAMAD PEMBA
Serikali ya
mapinduzi zanzibar imetakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika wanazifanyia suluhu
majumbani kwao kesi za udhalilishaji kwa watoto.
Hayo
yamesemwa na wanafunzi wa skuli ya chokocho wilaya ya mkoani pemba katika mkutano
wa kushajisha jamii juu ya umuhimu wa
kutoa ushahidi mahakamani kwa
kesi za udhalilishaji.
Wamesema bado wapo
wanafamilia wanashindwa kwenda
mahakamani kutoa ushahidi na kuzifanyia
suluhu wenyewe kwa wnyewe jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa udhalilishaji
hapa nchini.
‘’tunaiomba
serikali kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaoharibu ushahidi kwa
makusudi.
Kwa upande wake mwanafunzi isha hassan ibrahim kutoka skuli ya sekondari chokocho amesema wakati umefika kwa wazazi na walezi kuwa mstari mbele kuzisimamia ipasavyo kesi hizo ili kuona wabakaji wanatiwa hatiani.
Aidha amewataka wanafunzi hao kushuhulikia masomo
yao ili waweze kupata ufalu mzuri katika mitihani yao.
Comments
Post a Comment