WADAU WA KUPINGA UDHALILISHAJI WAWAPIGA MSASA WANAOSULUHISHA KESI ZA UDHALILISHAJI MAJUMBANI KWAO.


 

NA FATMA HAMAD PEMBA  12/4/2021.

Jamii imetakiwa kuondosha muhali na kuachatabia ya kufanya suluhu majumbani  kesi za udhalilishaji  jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa matendo hayo.

 Akitoa elimu kwa wanafunzi na wazazi huko skuli ya Muambe wilaya ya mkoani  juu ya athari za utdalilishaji  msaidizi wa sheria  shehia ya mkanyageni  Haji Shoka  amewataka wanafunzi  pamoja na wazazi kuzipeleka katika vyombo vya sheria kesi za udhalilishaji.

Amese licha ya elimu inayotolewa kwa jamii juu ya madhara ya  udhalilishaji  lakini bado kunabaadhi ya wazazi wanazifanyia suluhu majumbani kesi  hizo kwa kuhofia ugomvi katika familia zao hali ambayo inawakosesha haki  zao wahanga wa matendo hayo.

‘’Wazazi acheni ubishi kimbilieni kwenye vyombo vya sheria wakati unapotokea udhalilishaji’’ Alisema msaidizi wa sheria.

Amesema  wakati umefika kwa Wazazi na Walezi kushirikiana na vyombo vya sheria juu ya kesi hizi za udhalilishaji ili kuondosha unyama huu ambao wanaendelea kufanyiwa Watoto siku hadi siku.

Aidha amewanasihi wanafunzi wa skuli ya Muambe kutoa  tarifa kwa Walimu na wazazi wao pindi wanapoona udhalilishaji unafanyika  katika skuli zao bila ya woga wowote kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondosha matendo hayo kijijini kwao.

‘’Wanafunzi musimuogope mtu hatakama ni mwalimu, ni mjomba wako ukiona ana vitendo vibaya toa tarifa achukuliwe hatua’’ Alisema Haji Shoka.

Ameeleza Elimu ndio msingi wa maisha hivyo ni budi kuachana na tabia hatarishi na badala yake kushuhulikie masomo yao ili kupatikana Taifa lenye wataalamu katika Sekta mbali mbali ikiwemo Afya na Elimu.



Nao wanafunzi
  na wazazi wa Skukuli hiyo  wameitaka Serikali ya Mapinduzi kutoa Adhabu kali kwa wahalifu wanaofanya makosa hayo ili  kukomesha  udhalilishaji hapa Nchini.










 

 

 


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.