WANANCHI WAHIMIZWA KUWAPELEKA WATOTO VITUO VYA AFYA KUPATA CHANJO
Akizungumza
na Wandishi wa habari huko ukumbi wa Maabara Chake chake Pemba Afisa Mdhamini
wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Yakoub Mohd Shoka amesema
zoezi la utoaji wa chanjo litanza rasmi tarehe 26 hadi 30 mwezi huu katika
Vituo vyote vya Afya vilivyomo wilaya zote Visiwani hapa.
Amesema kila mwisho wa mwezi wa Nne ya kila mwaka, ni wiki ya chanjo
ya Afrika ambapo kwa Zanzibar wizara ya
Afya huadhimisha zoezi la utoaji wa
chanjo za kawaida kwa Watoto na akinamama ili kua na jamii isio na mambukizi
ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ‘’Chanjo huweka Jamii pamoja’’.
Amesema
lengo la Chanjo hizo ni kuhakikisha Watoto wote wanapatiwa, ili waweze
kuondokana na maradhi hatarishi ikiwemo Saratani ya mlango wa kizazi, Polio,
kifua kikuu, Surua, na kifaduro.
Amefahamisha
kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kufanya jitihada mbali mbali
za makusudi ili kuona Watoto wote wanaishi wakiwa na Afya nzuri.
Kwa upande
wake mratibu wa huduma ya chanjo za Mama
na Mtoto Pemba Bakar Hamad Bakar amesema licha ya juhudi mbali mbali
zinazochukuliwa na Serikali ili kuona Watoto wanaondokana na maradhi ya
mambukizi lakini bado wanajamii wanamuhali juu ya chanjo hizo kwa.
Hivyo amewahimiza
Watoto wote wenye umri wa miaka 14 kufika vituoni kupatiwa chanjo ili kujikinga na mambukizi ya maradhi ya Saratani ya mlango wa kizazi.
Comments
Post a Comment