MABARAZA YA YATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA WENYE SIFA

Wajumbe wa mabaraza ya Vijana Zanzibar wametakiwa kuchagua viongozi imara ambao wataendesha vyema mabaraza hayo.

Akizungumza na wajumbe wa mabaraza ya vijana kisiwani Pemba Afisa mdhamini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Salum Ubwa Nassor katika mkutano wa tathimini wa baraza hilo tangu lilipoanzishwa mwaka 2016 hadi 2021 huko Gombani Chake chake Pemba.

Amesema bila ya viongozi wenye sifa hawawezi kulifanya baraza kufikia katika maendeleo yaliokusudiwa katika kuanzishwa kwake.

‘’Niwaombe wajumbe mliopo kwenye baraza na mliostafu kutafuta wenye viti na makamo wapya ambao wataliendeleza baraza hilo’’ amesema mdhamin ubwa.

Akifafanua kua viongozi wa mabaraza yaliopita walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani waliweza kuongeza vijana wengi katika mabaraza yao.


Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la Vijana Zanziba Khamis Kheri Makoti amesema wameamua kufanya tathmini ya mabaraza ya vijana kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake katika kipindi chote cha uongozi wao tokea  kuanzishwa mwaka 2016 hadi 2021 kwa lengo la kuangalia maendeleo ya kiuchumi, Uzalendo na masuala ya kijamii.

Amesema lengo la tathmini hiyo ni kuona wajumbe wapya watakaochagulia kuendesha mabaraza ya vijana yajao kuwa wazalendo na wadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ambayo yanaendana na Serikali ya awamu ya Nane.



Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.