MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA WAWI CHAKE CHAKE PEMBA WAMEDHAMIRIA KINGARISHA SEKTA YA MICHEZO
SALIM HAMAD,PEMBA
MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Bakari Hamad Bakari pamoja na
Mbunge wa Jimbo hilo Khamisi Kassim Ali wamesema watahakikisha wanaiboresha
sekta ya michezo kwa kutengeneza miundombinu ya Viwanja ambayo imekuwa kero
kwenye Jimbo hilo.
Wakizungumza na wananmichezo katika hafla ya kukabidhi jezi
kwa timu mbali mbali za jimbo hilo Kisiwani hapa wamesema wanafahamu mazingira
ya Viwanja hususani katika kipindi cha masika mvua zinapo nyesha.
Mwakishi huyo Bakari Hamad Bakari alisema wanafahamu
changamoto za viwanja ambapo timu nyingi za jimbo hilo zimekuwa na viwanja
ambavyo sirafiki hasa zinaponyesha mvua za masika viwanja wao hujaa maji na
kusababisha kushindwa kufanya mazoezi.
Alisema mkakati wao ni kutengeneza Viwanja vitatu na
kuvifanya kuwa vya kisasa ili timu za jimbo hilo ziweze kucheza katika
mazingira mazuri kama timu nyengine za Tanzania bara.
Alisema tayari waliashaanza kutengeneza kiwanja Cha Ndugu
kitu kinachotumiwa na timu Machomane United na sasa wataendelea kutengeneza
uwanja wa Ngerengere kinachotumiwa na timu ya Hadrock inayomilikiwa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzani na kutengeneza uwanja wa Nyungunyungu uliopo Mkanjuni Chake
Chake.
‘’Tunadhamira kubwa ya kuzisaidia timu za Jimbo la Wawi kwa
kutengeneza Viwanja sasa tumeshatengeza Kiwanja kinachotumiwa na timu ya Machomane United na tunaendelea kutengeza
Viwanja vyengine kuona timu zinacheza
kwenye mazingira mazuri’’alisema Bakari.
Alisema hiyo ni moja na nyenzo muhimu ambayo anaamini itakapokamilika kutasaidia kuondosha changamoto za Viwanja zinazozikuba timu mbali mbali za Jimbo la Wawi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Khamisi Kasim Ali alisema wataendelea kuzisadia timu kila watakapopata wasaa ili kuona soka la Pemba,linaimarika.
Comments
Post a Comment