KOCHA wa timu ya Waawi Star Kasim Ali Kasim amesema atautumia mfungo wa ramadhani kwa kukifua kikosi chake ili kiwefiti katika michano ya ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba,itayoendelea tena mara baada ya mfungo wa Mwezimtukufu wa ramadhani.
KOCHA wa timu ya Waawi Star Kasim Ali Kasim amesema atautumia
mfungo wa ramadhani kwa kukifua kikosi chake ili kiwefiti katika michano ya ligi daraja la kwanza kanda
ya Pemba,itayoendelea tena mara baada ya mfungo wa Mwezimtukufu wa ramadhani.
Wawi Star ambayo ilishawahi kushiriki ligi kuu ya Zanzibar, msimu wa mwaka juzi iliyaanza
mashindano hayo kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mkoroshoni United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Gombani Kisiwani
hapa.
Akizungumza na Mwanaspoti Kocha huyo alisema licha kuwa
Vijana wake wapo kwenye swaumu lakini atakitumia kipindi cha mapunziko ya ligi kwa
kufanya mazoezi ya kufa mtu kuona wanafanya vizuri kwenye mzunguko wa pili.
Alisema katika mzunguko uliopita aliona udhaifu mkubwa
kwenye kikosi chake hasa katika sehemu
ya umaliziaji kiasi cha kumfanya kocha huyo kuamua kuutumia mwezi huu wa mfungo kukiandaa kikosi
chake.
‘’Kkipindi hichi cha ramadhani hatutolala tutahamasishana kufanya mazoezi kuona
yale mapungufu yaliyojitokeza katika mzunguko wa kwanza yanaondoka tuweze
kufanya vizuri kufanya vizuri katika mzunguko ujao’’alisema.
Katika hatua nyengine Kocha huyo aliwasifu waamuzi
waliochezesha mzunguko wa kwanza kwa kuchezesha vizuri kwa kila timu kupambana
kiuwezo wake .
‘’Ligi imenza vizuri
waamuzi walichezesha mzunguko wa kwanza watayafanya mashindano hayo kuwa na
ubora na yenye ushindani mkubwa na
kuepusha uvunjifu wa amani viwanjani uliokuwa unajitokeza vizuri hakuna
timu iliyokuwa inalalamika saana kuwa imeoneowa tunawaomba waamuzi wajitahidi
kuzifuata sheria za Soka ili kulinda
heshma zao na kuepusha na lawama viwanjani’’alisema.
Comments
Post a Comment