VILABU VYA DARAJA LA KWANZA KANDA YA PEMBA YATAKIWA KUJIPANGA KIMASHINDANI

 

SALIM HAMAD,PEMBA

KOCHA Mkuu wa timu ya Chipukizi Mwalim Mzee Ali Abdalla amezitaka timu zinazoshiriki ligi draraja la kwanza kanada ya Pemba,kujiandaa kiushindani ili kuhakikisha zinafanya vizuri katika mzunguko wa pili baada ya kupisha mfungo wa mwezi wa  ramadhani.

Akizingumza na Mwanaspoti Kocha huyo alisema katika michezo yote 12 ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa timu nyingi  zilionesha dhahiri kwamba hazikuwa na maandalizi ya kutosha hivyo zinahitaji kujipanga vizuri na kukuzakuitia ladha ligi hiyo.

Alisema ukiangalia kwenye matokeo timu nyingi zilikuwa zinatoka sare kiasi ya kwamba timu zinafanana kimatokeo ambapo alidai kuwa hicho ni kiashiria tosha kuonesha kwamba timu hazikuwa na maandalizi mazuri.

‘’Nidhahiri kwamba katika mzunguko ulimalizika timu nyingi hazikuwa na maandalizi ya kutosha zilishiriki tu kwani zilikuwa kila siku zinapokea taarifa ligi inaanza lakini haifanyiki jambo hilo limeziathiri sana klabu za Pemba ‘’alisema Mwalimu huyo.

Alisema inagawa baadhi ya timu zile ndogo kama Afrikana zilikuwa kidogo na ushindani ambazo zilikuwa na matayarisho kidogo zikiwa zinapanda sasa daraja kwani zilikuwa na hamu kubwa na mashindano hayo ndiyo kidogo zilijikaza kaza.

Alisema vilabu vikongwe vilivyoteremka kutoka ligi kuu ya Zanzibar, kama Jamhuri na Mwenge zilipoteza michezo yao ya kwanza kwa kufungwa na timu zilizopanda daraja zikitokea mkoa akitolea mfano Mwenge kufungwa na Africana magoli 3-1, huku Jamhuri ikilala kwa bao 1-0 kutoka kwa Yosso Boys.

Alisema walimu kwa sasa wanapaswa kufanya kazi ya ziada  kuziandaa timu zao kimbinu kisaikoloji kuhakikisha zinakuwa na matayarisho ya kutosha iwe tofauti na mzunguko uliopita ili ziweze kufanya vizuri kwenye mzunguko unaofuata.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.