TALAKA ZACHANGIA UDHALILISHAJI KWA WATOTO





Kukosekana kwa Malezi ya pamoja kati ya Baba na Mama ni chanzo kikubwa kinachopelekea Watoto kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ikiwemo Ulawiti na Ubakaji.

Akizungumza na Pemba ya leo Katibu wa kamati ya Madili kupitia baraza la Tasisi za Kislamu Zanzibar Abdala Mnubi Abasi amesema imebainika kuwa wanandoa wengi wanapoachana mzigo mkubwa wa malezi humuangukia mama peke yake hali ambayo kunakosekana kwa huduma bora kwa Watoto.

Amesema kukosekana kwa malezi ya pamoja ya Baba na Mama watoto hukosa  matunzo stahiki na kuamua kujiajiri wenyewe hali ambayo inasababisha kufanyiwa udhalilishaji.

‘’Inapovunjika ndoa   Watoto husambaratika kwani mababa hawatoi tena huduma’’, Alisema katibu wa madili.

Amesema imebainika kuwa wengi wafanywaji wa matukio hayo ni watoto ambao wamekosa malezi ya pamoja kutokana na wazazi wao kuachana.

Katibu huo amewataka wanajamii kuwa na subra wakati inapotokezea migogoro ya kifamilia na kutafuta suluhu mbadala ili kuepusha talaka za ovyo ovyo jambo ambalo litawafanya watoto kuishi  maisha ya amani na kuepukana na udhalilishaji. 




 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.