VILABU VYA DARAJA LA KWANZA KANDA YA PEMBA VYATAKIWA KUJIPANGA KIMASHINDANI
SALIM HAMAD,PEMBA
KOCHA Mkuu wa timu ya Chipukizi Mwalim Mzee Ali Abdalla
amezitaka timu zinazoshiriki ligi draraja la kwanza kanada ya Pemba,kujiandaa
kiushindani ili kuhakikisha zinafanya vizuri katika mzunguko wa pili baada ya
kupisha mfungo wa mwezi wa ramadhani.
Akizingumza na Mwanaspoti Kocha huyo alisema katika michezo yote
12 ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa timu nyingi zilionesha dhahiri kwamba hazikuwa na
maandalizi ya kutosha hivyo zinahitaji kujipanga vizuri na kukuzakuitia ladha
ligi hiyo.
Alisema ukiangalia kwenye matokeo timu nyingi zilikuwa
zinatoka sare kiasi ya kwamba timu zinafanana kimatokeo ambapo alidai kuwa
hicho ni kiashiria tosha kuonesha kwamba timu hazikuwa na maandalizi mazuri.
‘’Nidhahiri kwamba katika mzunguko ulimalizika timu nyingi
hazikuwa na maandalizi ya kutosha zilishiriki tu kwani zilikuwa kila siku
zinapokea taarifa ligi inaanza lakini haifanyiki jambo hilo limeziathiri sana
klabu za Pemba ‘’alisema Mwalimu huyo.
Alisema inagawa baadhi ya timu zile ndogo kama Afrikana zilikuwa
kidogo na ushindani ambazo zilikuwa na matayarisho kidogo zikiwa zinapanda sasa
daraja kwani zilikuwa na hamu kubwa na mashindano hayo ndiyo kidogo zilijikaza
kaza.
Alisema vilabu vikongwe vilivyoteremka kutoka ligi kuu ya
Zanzibar, kama Jamhuri na Mwenge zilipoteza michezo yao ya kwanza kwa kufungwa
na timu zilizopanda daraja zikitokea mkoa akitolea mfano Mwenge kufungwa na
Africana magoli 3-1, huku Jamhuri ikilala kwa bao 1-0 kutoka kwa Yosso Boys.
Alisema walimu kwa sasa wanapaswa kufanya kazi ya ziada kuziandaa timu zao kimbinu kisaikoloji
kuhakikisha zinakuwa na matayarisho ya kutosha iwe tofauti na mzunguko uliopita
ili ziweze kufanya vizuri kwenye mzunguko unaofuata.
Comments
Post a Comment