MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA WAWI WADHAMIRIA KINGARISHA SEKTA YA MICHEZO


 






SALIM HAMAD,PEMBA

MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Bakari Hamad Bakari pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Khamisi Kassim Ali wamesema watahakikisha wanaiboresha sekta ya michezo kwa kutengeneza miundombinu ya Viwanja ambayo imekuwa kero kwenye Jimbo hilo.

Wakizungumza na wananmichezo katika hafla ya kukabidhi jezi kwa timu mbali mbali za jimbo hilo Kisiwani hapa wamesema wanafahamu mazingira ya Viwanja hususani katika kipindi cha masika mvua zinapo nyesha.

Mwakishi huyo Bakari Hamad Bakari alisema wanafahamu changamoto za viwanja ambapo timu nyingi za jimbo hilo zimekuwa na viwanja ambavyo sirafiki hasa zinaponyesha mvua za masika viwanja wao hujaa maji na kusababisha kushindwa kufanya mazoezi.

Alisema mkakati wao ni kutengeneza Viwanja vitatu na kuvifanya kuwa vya kisasa ili timu za jimbo hilo ziweze kucheza katika mazingira mazuri kama timu nyengine za Tanzania bara.

Alisema tayari waliashaanza kutengeneza kiwanja Cha Ndugu kitu kinachotumiwa na timu Machomane United na sasa wataendelea kutengeneza uwanja wa Ngerengere kinachotumiwa na timu ya Hadrock inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzani na kutengeneza uwanja wa Nyungunyungu uliopo Mkanjuni Chake Chake.

‘’Tunadhamira kubwa ya kuzisaidia timu za Jimbo la Wawi kwa kutengeneza Viwanja sasa tumeshatengeza Kiwanja kinachotumiwa na timu ya  Machomane United na tunaendelea kutengeza Viwanja vyengine kuona  timu zinacheza kwenye mazingira  mazuri’’alisema Bakari.

Alisema hiyo ni moja na nyenzo muhimu ambayo anaamini itakapokamilika kutasaidia kuondosha changamoto za Viwanja zinazozikuba timu mbali mbali za Jimbo la Wawi.




Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo Khamisi Kasim Ali alisema wataendelea kuzisatia timu kila watakapopata wasaa ili kuona soka la Pemba,linaimarika.







Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.