WAZAZI WAPEWAMBINU.
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Kukosekana kwa
malezi ya pamoja
[zamani] ni moja
ya sababu inyochangia
kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa
matendo ya udhalilishaji
wa kijinsia katika jamii.
Hayo
yamelezwa na mratibu wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania tamwa ofisi ya Pemba Fathiya Mussa Said katika
kongamano la madhimisho ya asasi za kiraia
ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na
watoto huko micheweni mkoa wa kaskazini Pemba.
Amesema
licha ya elimu inayotolewa juu ya udhalilishaji lakini bado suala hilo
linazidi kuongezeka hivyo wakati umefika kwa wazazi kukachini ili kurudisha malezi ya zamani hali ambayo
itakua ni muarubaini wa hayo.
‘’kwa kweli
hali imekua tete jamani suala la kukaa
kila mtu na mwanawe imeshapitwa na wakati tukaeni tutafakari ni hatari sana’’
alieleza kwa masikitiko mratibu tamwa.
Kwa upande
wake afisa dawati la jinsia la wanawake na watoto wilaya ya micheweni Mohamed
Ali ameitaka jamii kuanzisha kamati za
madili katika shehia zao na kujiwekea sheria ndogo ndogo ambazozitawachukulia
hatua wale wote watakaobainika wanajihusisha na vitendo viovu.
Nae makamo mkurugenzi wa jumuia ya wasaidizi wa sheria wilaya ya micheweni Saleh Hamad Juma amesema ili kumaliza udhalilishaji ni vyema kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa madili ya kazi yake ili kuepusha malalamiko ya wananchi.
Nao wasaidizi wa sheria wilaya ya Micheweni wamevitaka vyombo vinavyoshuhulikia kesi za udhalilishaji kuzichunguza na kufanya upelelezi wa hali ya juu dhidi ya kesi hizo kwani kumekuwepo na baadhi ya wazazi huwafanya mabinti zao kama ni kitega uchumi na kuwabambikizia kesi wenziwao.
Kongamano hilo ni shamra shamra ya mishimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Comments
Post a Comment