WAZAZI WANYOOSHEWA VIDOLE
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Wazazi na
walezi wamenyoshewa kidole kwamba nawao ni moja ya chanzo kinachopelekea vijana kujiingiza katika matendo vya udhalilishaji wa kijinsia.
Wakizungumza
katika kongamano la maadhimisho ya asasi za kirai la siku 16 za kupinga ukatili wa wanawake na
watoto wanafunzi wa skuli ya msingi
mitiula wete Pemba wamesema wazazi wamekua hawana tabia za kufuatilia nyenendo
za watoto wao wakati wanapotoka kwenda madrasa pamoja na shuleni.
Wamesema
wapo baadhi ya wanafunzi wanatabia wanapondoka skuli hawafiki majumbani kwao
wanaishia vichochoroni hivyo wazazi kuweni makini juu ya watoto wenu msiwachie
fursa mpaka wakajisahau.
‘’Unapotoka
nyumbani mzazi hakuulizi unakwenda wapi na wala unarudi mda gani yani mda wako mwenyeo tu na safari zako hakuna
wa kukubugudhi’’ walisema wanafunzi.
Bimkubwa
Issa Omar mwanafunzi kutoka chuo cha afya wete amesema Kuwepo kwa masomo ya
ziada yasiyo na mpangilio yanachangia watoto kufanyiwa udhalilishaji.
‘’Sikuhizi mpaka wa watoto wa cheke chea na darasa la tatu wanakwenda masomo ya
ziada je tunawalinda vipi humo njiani wanamopita hebu tuliangalieni hili
jamani’’alisema Bimkubwa.
Akifungua
kongamano hilo katibu tawala wilaya
ndogo Kojani Makame Khamis amesema udhalilishaji hautondoka kwani bado wazazi hawajakua imara na imani thabit katika malezi
ya watoto wao.
‘’Wazazi
tukataka tusitake hatujakuwa na ikhlasi katika malezi mtu akishapeleka mapembe
na samaki aona ndo kazi imekwisha sivyo hivyo watoto wetu wanapotea’’ alisema
katibu tawala.
Comments
Post a Comment