VIJANA WAHIMIZWA KUFANYA KAZI KWA BIDII.

 

                         NA FATMA HAMAD FAKI PEMBA.

 Vijana wamehimizwa kujiingiza katika vikundi vya mazozi pamojana mpira wa miguu ili waweze kujipatia fursambalimbalizakimaendeleo.

Akizungumza na wanamichezo wampira wa miguu pamoja na wananchi mwanaharakati wakupambana na masuala ya udhalilishaji Khalfan Amour Mohamed katika shamra shamra ya kuelekea siku 16 ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto huko uwanja wa mpira wa michezo wa Majimaji uliopo Tumbe wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema udhalilishaji wa kijinsia umekua ni kilio kikubwa kwa wazanzibar waliowengi hivyo ni vyema vijana kujiepusha kukaa kwenye vigenge visivyo na tija kwao na badala yake wajikite zaid kwenye michezo.

‘’Niwasihi vijana wenzangu tuitumieni michezo, tuvitumieni vikundi vya mazoezi ili kujilinda na masuala ya udhalilishaj; alisema khalfan.

Aidha amewasisitiza kuondosha muhali na kuwatayari kutoa ushahidi wakati utakapotokezea udhalilishaji kwenye familia zao.

Kwa upande wake Tatu Abdala Mselem amewaasa vijana hao kuitumia mitandao ya kijamii kama ni sehemu moja ya kujipatia fursa za kimaendeleo na sio kuangalia mambo yatakaochochea kujiingiza kwenye udhalilishaji.

;Mitandao ya kijamii inafursa nyingi ila ukiitumia utakavyo itakupeleka hivyo hivyo utakavyo; alisema bi tatu.


Nao baadhi ya vijana walioshiriki kongamano hilo waliahidi kuifanyia kazi elimuwalioipata na kuwafundisha wengine ili waweze kujiepusha na matendo hayo.





Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.