WANAFUNZI WAPEWA MBINU ZA KUDHIBITI UDHALILISHAJI
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Wanafunzi maskulini
wameaswa kuepuka kufanya vitendo vya utovu
wa nidhamu na badala yake wafuatilie masomo yao kwanza ili waweze kufikia katika ndoto zao.
Hayo yamesemwa
na Afisa dawati wa jeshi la Polisi wilaya ya Micheweni Mohd Ali wakati
akizungumza na wanafunzi wa almadrasatul madyana imuslimina iliyopo wingwi mtemani wilaya ya micheweni
Kaskazini Pemba.
Amesema kesi
nyingi zinazoripotiwa zaidi ni za watoto
kuanzia miaka 14 hadi 16 jambo ambalo linapelekea
kukosa kuendelea na masomo yao.
‘’Sasahivi
ni wakati wa kusoma tu nyinyi msikubali kushawishika mkajingiza kwenye starehe mtakosa haki zenu za
elimu’’ alieleza afisa dawati.
Kwa upande
wake msaidizi wa sheria shehiya ya Micheweni Riziki Ali Hamad amewataka wanafunzi hao kutoa
tarifa kwa walimu wao ama wazazo wao wakati watakapoona kunakuwepo na viashiria
vinavyopelekea udhalilishaji ili viweze
kuchukualiwa hatua za kisheria jambo ambalo lipawaepusha na vitendo hivyo.
‘’ikiwa
mnafanyiwa vitendo vibaya msikae msikae kimya toweni tarifa hata kama ni mwalimu wako mkuu basi semeni
miogope’’ alieleza bi riziki.
Nao baadhi
ya walimu wa madrasa hiyo wamesema ni vyema Serikali ikangalia tena kwa umakini
sheria ya mtoto ili kuona adhabu inatolewa
kwa wote wawili mwanamme na mwanake
kwani sasahivi watoto wa
kike wanajifanya kama ni biashara.
Elimu hiyo
iliyotolewa madrasani hapo ni shamra shamra ya maaadhimisho ya siku 16 za
kupinga udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
Comments
Post a Comment