WADAU WA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI WAPEWA NENO

 

                                                         NA FATMA HAMAD,PEMBA

Wanaharakati pamoja na wadau mbali mbali wa kupambana na masuala  ya Udhalilishaji  wametakiwa kuendeleza mapambano dhidi ya vitendo hivyo ili kuhakikisha wanaondosha tatizo hilo ambalo limekua likiiathiri Jamii siku hadi siku.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Chama cha Wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar [TAMWA] Mzuri Issa Ali wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kuwasilisha ripoti ya utekelezaji wa majukumu yao kwa mwaka 2023 huko Ofisi za [TAMWA] Tunguu kisiwani Unguja.

Amesema vitendo vya udhalilishaji bado ni donda ndugu ambalo linaendelea kuiathiri Jamii, hivyo ni budi wanaharakati kujitoa kihali na mali kuifahamisha jamii kufahamu madhara ya udhalilishaji ili na wao waweze kuchukua hatua jambo ambalo litasaidia Watoto pamoja na wanawake kuishi kwa amani na matumaini.

‘’Niwambie wanaharakati wenzangu bado Jamii yetu inathirika na vitendo vya udhalilishaji, hivyo basi tusichoke kupiga kelele,tusivunjike moyo tuendeleekupambana,alisema.

 Wakichangia baadhi ya wadau walioshiriki mkutano huo walisema ili kufikia lengo la kuondosha Udhalilishaji Nchini ni wakati kwa watendaji wa vyombo vya kisheria ikiwemo Polisi, Mahakama, kutekeleza majukumu yao kwa uwadilifu na kuwa na ikhlasi ya hali ya juu ili kuona haki inatendeka jambo ambalo litaepusha malalamiko katika jami.

‘’Kama vyombo vya maamuzi havitobadilika na kufanya kazi zake kwa moyo wa uwadilifu  basi tutaendelea kuimba tu hatutofikia popote,walieleza wadau.

 Akiwasilisha ripoti  juu ya masuala ya udhalilishaji mwaka 2023 Mratibu wa Chama cha wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar Ofisi ya Pemba Fat hiya Mussa Said alisema bado suala la Rushwa muhali katika jamii limeonekana kuota mzizi, jambao linalopelekea kesi za udhalilishaji kuondolewa Mahakamani na udhalilishaji kuongezeka.

 Jumla ya kesi 220 za udhalilishaji zimeibuliwa na wanamtandao wa kupambana na udhalilishaji Zanzibar, kwa upande wa Pemba  ni 94, Unguja 126, ambapo 78 zipo Polisi zinaendelea na upelelezi, 19  zipo DPP, 20 zinaendelea Mahakamani, 8 zimeondolewa mahakamani, 44  zimepata uwamuzi na 51 zimemalizika kwa makubaliano.
 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.