kijana huyu mwenye ulemavu wa viungo ashindwa kwenda skuli kwa kukosa kibaskeli cha maringi mawili
Licha ya juhudi zinazochukuliwa na Serikali pamoja na Asasi mbali ili kuona watu wenye ulemavu na wao wanapata haki zao stahiki, lakini bado watu hao wanaendelea kukumbana na changamoto kadhaa na kupelekea kudumaa kwa maendeleo yao.
Hayo yamebainika kwa Kijana Anifu Jeilani Issa mwenye ulemavu wa Viungo (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano Skuli ya Msingi Ole Wilaya ya Chake Chake Pemba, kushindwa kuhudhuria Skuli kwa kukosa Kibaskeli cha magurudumu mawili.
Akizungumza kwa masikitiko Mama Mzazi wa Mtoto huyo huko Nyumbani kwake Ole Mihogoni amsema ni Zaidi ya miezi minne hivi sasa mototo wake Anifu hajahudhuria Skuli kuungana na wenzake kusoma kufuatia changamoto hiyo.
‘’ alikua nacho kigari lakini sasahivi kimeharibika, jambo ambalo linapelekea kukosa masomo yake’’ Alisema mama mzazi
Hivyo mama huyo amewaomba wahisani pamoja na wasamaria wema kupatiwa msaada wa kigari ili kuweza kushiriki kikamilifu katika masomo yake kwa vile hivi sasa anashindwa kuhudhuria kwa kukosa kibaskeli cha magurudumu mawili.
‘’Naomba msaada nipatiwe kibaskeli mtoto wangu aendeleze masomo yake ili aweze kutimiza ndoto zake.
Nae Mratibu wa Kitengo Cha Elimu Mjumuisho kutoka Wizara ya Elumu na Mafunzo ya Amali Kisiwani Pemba,Halima Mohd Khamis amesema Kitengo hicho kimekuwa kikichukua juhudi mbali mbali katika kuwasaidia watu wa aina hiyo lakini bado wanashindwa kulimaliza tatizo hilo kutokana na uhitaji wa Vifaa hivyo kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Comments
Post a Comment