UMASKINI WAPELEKEA WATOTO 6 WENYE ULEMAVU WA AKILI NA VIUNGO KUSHINDWA KUPATA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII

Wazazi wa watoto sita wenye ulemavu wa akili na viungo huko Kinyasini Mikarafuuni Wilaya ya Wete Pemba wamewaomba wasamaria wema kuwapatia msaada  ili kuweza kuwahudumia watoto wao, kwani kwa sasa wanashindwa kutokana na hali ngumu waliyonao jambo lililosababisha  kuwakatisha masomo.

Akizungumza na wandishi wa habari huko nyumbani kwake  Kinyasini Wete  baba mzazi wa watoto hao Saleh Juma Saleh ambapo ameanza kwa kueleza faraja  alioipata huko nyuma wakati watoto hao wakiwa ni wadogo kwa kufikwa na baadhi ya wahisani pamoja na viongozi wa serikali.

‘’Kipindi cha nyuma nashukuru walikuja watu wengi ikiwemo Serikali kuniona hali yangu na kunifariji, ila kwa sasa ni nadra na hali imezidi kuwa ngumu kwangu, alisema baba watoto.

Amefahamisha kuwa awali walikua wanasoma Shule ila kwa sasahivi wameshindwa kuendelea tena kutokana na ugumu wa maisha.

‘’Nimewakatisha masomo kutokana na uwezo,  Gari ipo ila sina mafuta ya kutia  kila siku na kuwapelekea shule,  na hivi saivi gari imelala bandani haina mafuta’’ Alieleza baba watoto.

Alifahamisha kuwa mda mwingi anatakiwa kubaki nyumbani kwa ajili ya kulea watoto hao, hivyo anashindwa hata kutoka na kwenda kutafuta Rizki jambo linasababisha maisha yao kuzidi kuwa magumu.

‘’Sasa Hivi  watoto  hawa wanahitaji ukae nao kwa ukaribu,  kwani wengine tayari wameshatimia umri wa utuuzima,  wanahitaji uangalizi wa hali ya juu ili kuwakinga na vitendo vya udhalilishaji,’’Aliendelea kueleza baba.

Aidha baba huyo amesema Kuwa  anakumbana na changamoto kubwa ya kuwapatia matibu watoto wake hao  walemavu sita pindi wanapoumwa.

‘’Wanapoumwa huumwa wote kwa pamoja nashindwa kuwapeleka Spitali wote, na kuwanunulia dawa wote  nashindwa sina uwezo,’’ Alisema baba.

Miongoni mwa viongozi waliofika kuwaona watoto hao katika mwaka 2013, ambapo watoto hao wakiwa bado ni wadogo ni aliyekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Marehemu Maalim Seif Sharrif Hamad.

Licha ya kuwa na ulemavu wa akili watoto hao ambao  wanaume  ni wawili, [2]  na
wanawake ni  wa nne [4]  pia wana ulemavu wa viongo na wanapotembea  kutumia miguu na mikono. 


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.