RUSHWA BADO NI TATIZO KWA WAGOMBEA WANAWAKE KISIWANI PEMBA.







Wanawake wagombea Kisiwani Pemba wapaza sauti zao kwa vyombo vya habari juu ya Kuepo kwa rushwa katika vyama vya siasa  kipindi cha uchaguzi mkuu, kikwazo ambacho kinapelekea wanawake  hao  kushindwa kufikia malengo yao.

Akizungumza  kwa masikitiko Hadia Omari Dadi katika mkutano wa uhamasishaji wa mwanamke kugombea nafasi za uongozi, huko Wingwi wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba alisema  unapofikia wakati wa uchaguzi suala la rushwa hujitokeza kwa wingi katika vyama jambo ambalo linawakosesha wanawake wenye kipato duni kushindwa kujinyakulia nafasi mbalimbalizauongozimajimboni.

Alisema inaonekana wengi wanaopata nafasi hizo ni wale wenye nacho,auwaleambaotayariwalishakaakwenyeuongozikwakipinchama.

‘’Mimi mwenyewe binafsi nishagombea mara tatu ila kwa sababu ni masikini, sina pesa nimeshindwakupatanafasiyoyoteilekutokanasinauwezo,’’Alisemabia.

Alifahamisha kuwa Rushwa ni adui mkubwa anekwamisha maendeleo, hivyo tunaishauri  Serikali  ya Mapinduzi kujipanga upya katika mwaka 2025 kupambana na viongozi wa vyama vya siasa ili kuona uhalifu huo umeondoka na kuona wanyonge nawao wanapata nafasi. 

Sambamba na hilo  aliitaka pegao kutoa elimu kwa Viongozi wa vyama vya siasa kutoa fursa kwa wale ambao wanasifa za uongozi nasio kumchagua mtu kwa sababu tu ana pesa zake, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

Akichangia katika mkutano huo Khamis Mohd Nassor pia alisema kuwa ni kweli wanawake wengi wa vijijini wanaishi katika mazingira magumu, lakini bado ile elimu hasa  ya kujiingiza katika uongozi  haijawaingia ipasavyo, jambo ambalo linawafanya wanaume kujichukulia fursa mbali mbali za kimaendeleo.

Nae mmoja wa wahamasishaji  wa mwanamke kugombea nafasi za uongozi Khalfan Amour Mohd alisema lengo la mkutano huo ni kuwafahamisha Wanawake kufahamu kuwa uongozi ni suala la mwanamke na mwanamme, na sio tu kama jamii inavyodai mwanamke hafai kuwa kiongozi.



Mkutano huo ni muendelezo wa mikutano ya uhamasishaji mwanamke kuwa kiongozi uliyoandaliwa na jumuia ya Pegao kwa kushirikiana na Chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [Tamwa]






Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.