WANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUANDIKA HABARI ZA VIJIJINI.
Afisa
mdhamini wizara ya habri Vijana na Michezo Salum Ubwa amewataka wandishi wa
habari kujikita zaid Vijijini katika
kuandika habari zao ili kuibua matatizo yanayo wakabili wananchi wa maeneo
hayo.
Hayo
ameyasema katika Kongamano la uhuru wa kujieleza upatikanaji wa habari,
mitandao ya kijamii na uandaaji wa maudhui kwa vijana na majukwaa ya maendeleo
kwa vijana huko Camail Chake chake Pemba.
Amesema vyombo
vya habari ndio msemaji wa wasio na sauti, hivyo ni budi kwa wandishi wa habari
kujitoa na kujituma ili kuona wananchi wa vijijini nawao wanapata fursa ya kuzungumza na vyombo vya habari kutoa kero zao na mamlaka husika na kuona wanazitekeleza.
‘’Wandishi msiishie
tu mjini nendeni vijijini kuna kero nyingi zinawakumba wananchi’’ Alisema afisa
mdhamini.
Amesema wananchi
wengi wa vijijini wanaendelea kuishi katika matatizo kutokana na kukosa taluma na
taratibu za ufuatiliaji wa shida zao kwa
vyombo husika jambo ambalo linapelekea kukosa haki zao.
Akiwasilisha
mada ya uhuru wa kujieleza na kupata
habari mkufunzi wa mafunzo hayo Haji Nassor Mohd amewashauri vijana kuvitumia
vyombo vya habari wakati wanapofanya shuhuli zao ili waweze kutambulika jambo
ambalo litawasaidia kupata fursa mbali mbali za kimaendeleo.
Baadhi
ya wandishi walioshiriki mkutano huo
wamesema bado jamii haijakua na mwamko wa kuvitumia vyombo vya habari kutoa
malalamiko yao kutokana na mila na desturi walizo nazo vijijini kwao.
Comments
Post a Comment