JUMUIA YA WATU WASIONA [ZANAB] PEMBA WAOMBA MSAADA
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Jumuia ya
watu wasiona [Zanab ] wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba imeitaka
Serikali pamoja na watu wenye uwezo kuwapa msaada wa kuwajengea jingo la Ofisi yao ili
kuwaondoshea usumbufu kwa wanajumuia hao.
Akizungumza
na mwandishi wa habari mwenyekiti wa jumuia hiyo Suleimana Mansour Suleiman
huko ofisini kwake Chake chake Pemba amesema
wanachangamoto kubwa ya uhaba wa vyumba katika jingo lao.
Amesema
Ofisi yao inawafanyakazi mchanganyiko wa
watu tofauti wakiwemo watu wenye ulemavu wa Ngozi, wenye ulemavu wa viungo
na wasiona lakini wanachumba kimoja tu hawana sehemu
nyengine ya kufanyia shuhuli zao za
kiofisi.
Amefafanua
kuwa unapofika wakati wa sala wanalazika wengine kukaa nje na kupishana kwa ajili ya kutekeleza ibada ya sala.
‘’Jengo letu ni dhaifu, Tunachumba kimoja tu
hatuna hata chumba cha stara, ukiangalia tupo mchanganyiko wanawake na
wanaume’’, Alisema
mwenyekiti.
Samba mba na
hilo mwenyekiti huyo ameeleza kwa masikitiko
makubwa wanakabiliwa na changamoto
ya ukosefu ya huduma ya choo katika ofisi yao.
Amesema
wanalazimika kutumia huduma ya vyoo vya jirani wakati wanapokwenda kufanya haja
zao hali ambayo inapelekea wafanyakazi
wake kushindwa kuhudhuria kazini kwa
wakati.
Tunakwenda
choo cha Mkuu wa wilaya, Hospital na ikitokezea wenyewe ikiwa hawapo kazini tunahangaika hatuna pakujisaidia,
hivyo tunaomba msaada tujengewe japo vyumba viwili tu.
‘’Ivi
Serikali sisi watu wenye ulemavu haituoni tumekosa nini sisi,ata pakwenda haja
ndogo hatuna’’ Alisema mwenyekiti wa Zanab.
Mapema Mratibu wa Idara ya watu wenye ulemavu Pemba Mashavu Juma Mabrouk amesema
atafanya jitihada ya kuwasaidia walemavu hao ili waweze kuondokana na
changamoto hiyo.
Mkuu wa
wilaya ya Chake chake Abdala Rashid Ali
amefahamisha kuwa ofisi yake iko kwenye harakati za kutafuta msaada
mbalilimbali japo kwa wahisani wengine kuhakikisha wamejengewa majengo ili
kuona kilio cha walemavu hao kimepatiwa
ufumbuzi.
‘’Ni kweli
ofisi hiyo inachangamoto ya majengo pamoja na choo,ila tunawaomba wavute subra tupo mbioni kulitafutia ufumbuzi,’’ Alisema
mkuu wa wilaya.
Comments
Post a Comment