WANDISHI WAONYWA KUEPUKA KUANDIKA HABARI ZA UCHOCHEZI
Wandishi wa habari wametakiwa kuepuka kuandika habari zisizo na mizania na zenye viashiria vya uchochezi ili kusaidia kuepusha kutokea kwa migogoro isiyo ya lazima katika jamii.
Wito huo
ulitolewa wakati wa mafunzo ya kujenga amani na utatuzi wa migogo kwa waandishi
wa habari kisiwani Pemba yalioendeshwa na shirika la kimataifa la utatuzi wa
migogor la SEARCH FOR COMAN GROUND kupitia mradi wa Dumisha amani Zanzibar.
Akizungumza
na wandishi wa habari katika mafunzo ya
kutatua migogoro kwa njia shirikishi yenye lengo la kudumisha amani Husein Faraji Sengu amesema lengo la mradi ni kusadia kutatua migogoro ya kisiasa hususani
mara baada ya kumalizika uchaguzi Zanzibar.
Amesema
uzoefu unaonyesha kua Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi kumekua kukitokea
athari nyingi za kisisiasa ambazo zinatokana na uchaguzi ikiwemo migogoro kwa
matabaka tofauti ambayo ikiachiwa iendelee inaweza kuondosha amani ya zanziba
iliopo.
Amesema wakati
mwengine vyombo vya habari vimekua vikinyooshewa vidole ndio kusababisha kuchochoa au kukuza mizozo inayo
tokea katika jamii kutokana na kuhabarisha visivo sahihi ikiwemo kuandika kwa
kuegea upande mmoja.
Amesema
uandishi wa habari wa namna kama hiyo unasababisha jamii kukosa imani na
muandishi na chombo chake cha habari sambamba Nchi kuingia katika migogoro, hivyo amesema niwakati
sasa waandishi kubadilika na kuweka umakini wa
hali ya juu wakati wa kuandika na
kuripoti taarifa.
Amesema ni
vyema kwa wandishi wa habari kutumia kwa uweledi ujuzi wao na kuzingatia madili
ya habari wakati wanapokua katika majukumu yao ili kuona wanandika habari zenye
ukweli na zenye kuleta mabadiliko chanya kwa jamii na nchi.
‘’Wandishi
wa habari acheni kuandika habari zisizo zingatia maadili ya habari, epukeni
kuandika habari zenye uchochezi ambazo hazina maslahi kwa umma’’, Alisema
Meneja.
Haji Nassor Mohd kutoka mtandao wa pemba to day ambae ni miongoni mwa wandishi walioshiriki mafunzo hayo amewataka wandishi wenzake kuyatumia vyema mafunzo katika kuandika habari ili kuona wanaleta mabadiko sahihi ndanin ya jamii.
Comments
Post a Comment