SHAHIDI AISHANGAZA MAHAKAMA



NA FATMA HAMAD PEMBA 

MTOTO mwenye miaka 17 ambae ni shahidi, ameishangaza mahakama ya Mkoa ‘B’ Chake chake kwa kuiambia kua alimtaja mtuhumiwa Ibrahim  Khamis Abdalla kwa shindikizo la wazazi wake tu, kwamba ndie aliempa ujauzito, lakini yeye hahusiki na ujauzito huo.

Akitoa ushahidi wake  mbele ya mahakama hiyo, shahidi huyo ameeleza kuwa wazazi walimlazimisha kumtaja mtuhumiwa huyo,  kwanindie waliekuawa kimdhania. 

Alidai kuwa mtuhumiwa ni rafiki yake wa mudamrefu, ingawa sie aliyempa ujauzito na aliamua kumtaja kutokana na sindikizo la wazazi wake.

“Nakataa ujauzito sijapewa na Ibrahim nilipewa na mwanamme ambae tukikutana tu kwenye kampeni na wala si mfahamu kwao anapoishi,’’ alidai.

Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka [DPP] Ali Amour Makame alidai kutokana na maelezo ya shahidi huyo kwa upande wao wanafunga ushahidi.

‘’Mheshimiwa tunafunga ushahidi wa kesi hii na tunaiachia mahakama yako iweze kutoa maamuzi,’’ alidai.

Hakimuwamahakama hiyo Lusiano Makoye Nyengo amekubaliana na taarifa ya Mwendesha mashtaka na aliamua kuigharisha hadi tarehe 26/7/ mwakahuu kwa ajili yauamuzi.

Imedaiwa mahakamani hapo siku, tarehe na mwezi usiofahamika mwakajana ,mtuhumiwa Ibrahim Abdalla Khamis miaka 20 nyakati za mchana eneo la Kipapo wilaya ya Chakechake, alidaiwa kumbaka mtoto17.

Kufanyahivyo ni kosa kinyume na sheria kifungu cha 108 [1] [2] [e] na 109[1] cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.




Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.