JESHI LA POLISI LA DAIWA KUFANYA SULUHU KESI ZA UDHALILISHAJI
Wadau wa
kupinga ukatili na udhalilishaji wa
kijinsia kisiwani Pemba wamelalamikia juu ya uwepo wa baadhi ya Askari wanaozifanyia suluhu kesi
za udhalilishaji.
Akizungumza
katika mkutano wa uwasilishaji wa ripoti
ya utekelezaji wa mradi wa
kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia msaidizi wa sheria kutoa mkanyageni mkoani
pemba Shaban Juma Kassim huko ofisi za chama cha Wandishi wa habari Wanawake
Tanzania [TAMWA] Chake chake amesema kazi ya askari ni kufanya upelelezi
tu na sio kutoa suluhu.
Amesema wapo
baadhi ya askari huwataka wazazi wanaokwenda
kuripoti kesi za udhalilishaji kuzimalizia vituoni tu na wasiende
mahakamani.
‘’Bado
wenzetu wa Jeshi la polisi wanaturejesha nyuma hawajakuwa tayari kukomesha
udhalilishaji,’’Alisema msaidizi wa sheria.
Hivyo
amewataka wazazi wa wathirika wa matukio hayo wasikubali suluhu bali wasimame
kidete kutoa ushahidi ili kuona kesi zao zimepatiwa hatiani.
Kwa upande
wake Haji Shoka Khamis msaidi wa sheria kutoka Chokocho amesema udhalilishaji utaendelea
kuwakumba wanajamii kwani bado hakuja kuwepo na sauti ya pamoja [mashirikiano]
kati ya Wananchi, Wadau wa kupinga udhalilishaji pamoja na taasisi za kisheria
ikiwemo Jeshi la Polisi.
Baadhi ya
wazazi wa wathirika wa udhalilishaji walioshiriki mkutano huo wamesema bado
kumekuwepo na udhoroteshwaji wa uwendeshwaji wa kesi mahakamani jambo ambalo
linawafanya wananchi walio wengi kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi.
‘’Tunaumia
jamani mtu anatoka muambe anakuja chake, akifika anambiwa mjoo kesho mjo kesho
kutwa tunaumia hatuna nauli
tuwanyonge,’’ Alidai mzazi.
Mapema
mrajis wa mahakama kuu Chake chake Abdul razzak Abdul kadir Ali amesema wengi
wanaofanyiwa matendo hayo ni watoto kuanzia mika 18 hadi 15 ambapo tayari
wameshajielewa, hivyo amewataka wazazi kuweka utaratibu kama vile zamani wa
kuwapekuwa watoto wao wakati wanaporudi safari zao, kwani kufanya hivyo
kutawatia hofu na kujiepusha kufanya matendo maovu.
Nae mratibu
wa chama wa wandishi wa habari Wanawake Tanzabia [TAMWA ofisi ya Pemba Fathiya
Mussa Said amewapongeza wadau hao kwa kazi kubwa walioifanya juu ya ufuatiliaji
wa kesi hizo, hivyo amewataka kuongeza nguvu ya mapambano ili kuona
udhalilishaji umendoka na jamii kubaki salama.
Comments
Post a Comment