ZAEKA YATAKIWAN KUHAMIA KATIKA OFISI ZA VYAMA VYA SIASA WAKATI UNAPOFIKIA KIPINDI CHA CHAGUZI
Mamlaka ya kuzuia Rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar [ZAEKA] imetakiwa kuelekeza nguvu zao za uchunguzi katika vyama vya siasa wakati unapofikia uchaguzi mkuu wa Zanzibar ili kuwakamata na kuwachukulia hatua wale ambao watabainika kutoa rushwa kwa ajili ya kupata nafasi za uongozi Majimboni.
Wito huo
umetolewa na baadhi ya Wanawake waliogombea nafasi mbali mbali za uongozi
katika uchaguzi mkuu uliopita 2020
wamesema wakati unapofika kipindi cha uchaguzi rushwa imekua ikitawala kwa
kiasi kikubwa katika vyama siasa nchini.
Wamefahamisha
kuwa nafasi za uongozi majimboni asilimia kubwa huchukuliwa na wale wenye pesa
tu, jambo ambalo linawakatisha tama wanawake masikini wenye nia ya kugombea
kushindwa kuwania nafasi hizo.
‘’Tuna iomba
zaeka itende haki, katika kazi yao ya kupambana na rushwa na uhujumu uchumi kuwachukulia
hatua wale wote ambao wanatumia nguvu ya fedha kama njia ya kupata madaraka,’’
Walisema wanawake wagombea.
Aidha
wamesema endapo kwa viongozi wa vyama vya siasa hawatobadilika na kuliondosha
suala la rushwa kutakuja kukosekana kwa
viongozi wanawake majimboni hususan wenye uwezo mdogo wa kifedha.
Nae Afisa wa
mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar Zaeka Kisiwani Pemba Suleiman
Ame Juma amesema rushwa si katika
chaguzi tu, hivyo amewataka wagombea wanawake kushirikiana na mamlaka hiyo
kutoa ushahidi ili kuwakamata wale wote wanaofanya matendo hayo.
Comments
Post a Comment