SHAHIDI APELEKEA KESI KUGHAIRISHWA.


 

Kutokuwepo kwa shahidi  kumesababisha hakimu wa Mahakama ya Mkoa B  iliopo Chake chake kughairisha kesi ya kuingilia kinyume na maumbile inayomkabili kijana Ayoub Mohd Hamad mwenye umri wa 18 mkaazi wa Likoni kengeja  Wilaya ya Mkoani Pemba.

 Baada ya mtuhumiwa huyo kupanda kizimbani akisubiri kusomewa shitaka lake, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka [DPP] Ali Amour Makame  amesema leo walikua wasikilize  shahidi ambae ni askari mpelelezi ila hakufika mahakamani kwani hayupo kazini yupo likizo.

‘’Mheshimiwa hakimu tunaomba uipangie sikunyengine ili tumuombe  shahidi wetu aje kutoa ushahidi hata kama amesafiri,’’ Alidai DPP.

Hakimu wa mahakama hiyo Lusiano makoe nyengo amekubaliana na ombi hilo na kesi hiyo itaendelea tena tarehe 26/7/mwaka huu.

Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo siku ya tarehe 23/2/2021 majira ya 5;30 asubuhi, huko Likoni Kengeja wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Alimuingilia kinyume na maumbile ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifu cha 133 [a] cha sheria ya adhabu sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.