NA FATMA HAMAD PEMBA.Ugeni
kutoka falme za kiarabu [Dubai] umeahidi kusaidi vifaa vya
tiba kama vile vya upasuaji, usafishaji wa figo, Exray, vifaa vya uchuguzi wa magonjwa ya
akinamama na watoto, na huduma nyengine mbali mbali za matibabu katika
hospitali za Wilaya Kisiwani Pemba.
Waziri wa Afya, Ustawi
wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amesema ahadi
hiyo imefuatia ziara ya kutembelea hospitali hizo iliyofanywa kati ya uongozi
wa wizara ya afya na Ugeni huo kujionea hali halisi ya utoaji wa huduma za
afya katika hospitali ya Wete, Micheweni na Vitongoji pamoja na kusikiliza
changamoto zilizopo.
Amesema baada ya
kuwatembeza na kujionea katika hospitali hizo, Ugeni huo umejionea mahitaji
ambayo yanahitajika ambapo wameyachukua na kwenda kuyafanyia kazi pamoja
na kuahidi kurudi baada ya miezi
michache nayale ambayo yatashindwa kutekelezwa na ugeni huo wataangalia namna
ya kuomba msaada kwa wahisani wengine.
‘’Atahakikisha
ametekeleza ahadi aliyoiweka japo kuomba misaada kwa wahisani wengine’’ Amesema
Mazrui.
Ameeleza kuwa lengo la
ugeni huo ni kuwasaidia wazanzibar katika masuala ya afya, hivyo ameitaka
Wizara ya Afya kumpa mashirikiano ili kuona alilolikusudia limefanikiwa kwa
maslahi ya Wananchi.
Akizungumza Ndugu Ahmed Alfrsy ambaye
aliongozana familia yake katika ziara hiyo amesema lengo ni kusaidia kutatua
changomoto ya vifaa vya tiba kwenye hospitali hizo ili huduma ziweze kupatikana
kwa wepesi bila ya kutumia gharama kubwa ambapo wengine wanashindwa kuzimudu.
Mmoja kati ya
madaktari dhamana kisiwani Pemba Dr.
Sharriff Hamad Khatib kutoka hospitali ya Vitongoji amesema wana imani
kubwa na ujio wa ugeni huo kwa vile umeahidi kusaidia upatikanaji wa vifaa
muhimu vya kutolea huduma katika hospitali zao.
Katika Ziara hiyo ya
Siku moja ugeni huo ulipata kutembelea hospitali za Vitongoji na Micheweni
Cottage na Hospitali ya Wete sambamba na kutembelea kwenye kijiji cha Shumba
Mjini.
Comments
Post a Comment