Wananchi nendeni mkaripoti kero zenu
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Mkuu wa
wilaya ya Wete Hamad Omar Hamad amewataka
wananchi wa mkoa wa Kaskazini Pemba kujitokeza kwa wingi katika kambi ya utoaji
wa huduma ya Msaada wa kisheria ili waweze kupeleka matatizo yao na kupatiwa
ufumbuzi.
Mkuu huyo ameyasema
hayo huko Micheweni wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud amesema Kambi hiyo ya siku
tatu itawasaidia Wananchi kupata huduma na pia kujua wapi waripoti malalamiko
yao.
Amesema Jamii
imekua ikikabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo ya Ndoa, Ardhi,Mirathi, na
Udhalilishaji hivyo ni wakati wananchi kuitumia fursa hiyo ili kuweza kupatiwa
msada wa kisheria.
‘’Kambi hiyo
itajumuisha Wanasheria, watoa huduma ya msaada wa kisheria hivyo tuwatumieni kwani ni bure hakuna malipo yoyote,’’alisema.
Kwa upande
mwengine Hamad amewataka Wandishiwa Habari kutumia kalamu zao kwa kuwafahamisha
wananchi ili waweze kufahamu na kujitokeza kwenye kambi hiyo.
Amesema uwepo
wa Mswaada wa kisheria ni suala mtambuka
kwani kutasaidia upatikanaji wa huduma za kisheria kwa Jamii.
‘’Tunafahamu
kuna watu hawajui hata pakukimbilia wala pakuanzia wakiwa na matatizo, hivyo
kambi ii itakuwa ni Faraja kwao,’’ anasema.
‘’Hakuna
kuachwa mtu nyuma tutahakikisha kila mzanzibari anapata haki ya kisheria na
anazimtambua sheria,ameeleza.






Comments
Post a Comment