Wanaume msizitelekeze familia zenu
NA FATMA HAMAD, PEMBA,
Afisa mdhamini Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Hafidh Ali Mohamed amewahimiza wazazi hussusan wa kiume
kusimamia majukumu yao ya kutunza na kulea familia zao ili kuwalinda watoto na
vitendo viovu ikiwemo udhalilishaji na ujambazi.
Afisa
huyo ametoa wito huo wakati akifungua mafunzo ya siku moja yanayohusu
kuwashirikisha wanaume katika malezi kwa Wasaidizi wa Sheria huko Makonyo Chake
chake Pemba.
Alisema
wanaume ndio wenye jukumu kubwa la kuhudumia familia zao, hivyo endapo hawatofuata
vyema wajibu wao huo kutapelekea
kupatikana kwa watoto wa mtaani pamoja na udhalilishaji kwa watoto.
‘’Niwasihi
wazazi wenzangu wa kiume sisi ndio wenye dhamana za kutoa matunzo, hivyo
tusizitelekeze familia zetu tutasababisha matatizo,’’alisema mdhamin.
Aidha
aliendelea kuwasihi wazazi kuwa na subra katika ndoa zao ili kuepusha talaka,
kwani hilo ni moja ya sababu inayochangia watoto kudhalilishwa.
‘’Watoto
wengi wanaokosa malezi ya pamoja ya Baba na Mama mara nyingi hukosa haki zao
ikiwemo Elimu pamoja na matunzo,na mwisho wa siku hupata udhalilishaji,’’alieleza.
Mapema
Afisa mdhamini wizara ya Katiba, Sheria na Utawala bora Halima Ali Khamis
aliwataka Wasaidizi wa Sheria kuendelea kuielimisha Jamii kulea woto wao katika
malezi ya pamoja ili kuweze kupatikana kwa kizazi chenye maadili mema.
‘’Jamani
kwa kweli hali ni mbaya, tuifahamisheni jamii kwamba mtoto asiwe wa mtu mmoja
tu bali alelewe na jamii huenda yakapungua hayo matendo maovu vijijini
mwetu,’’alisisitiza.
Aidha
aliendelea kusema kuwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia bado vinaendelea
kutokea katika jamii, hivyo wasaidizi wa Sheria mnadhima kubwa ya kuielimisha
Wananchi kuongeza kasi ya kupiga ita matendo hayo.
‘’Jamani
tusidharau vitendo vya udhalilishaji bado vipo,tuendeni kutoa elimu ili jamii
ichukuwe tahadhari ili tujikinge navyoalieleza,’’Halima.
Kwa
upande upande wake Mkurugenzi Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Hanifa
alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wasaidizi wa Sheria ili
waweze kuielimisha Jamii kusimamia vyema majukumu ya familia zao.
Nao
baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema ipo haja kwa wasaidizi wa Sheria
kufundishwa lugha za alama, jambo litalopelekea watu wenye ulemavu nawao kupata
haki ya msada wa kisheria pindi wakikutwa na matatizo.
Comments
Post a Comment