Vijana Pemba waliojiajiri ufugaji Kaa wasahau ajira ya Serikali

 

  NA FATMA HAMAD PEMBA,

Vijana wameonywa  kuepuka kukaa katika vigenge viovu ,na badala yake wajiunge  na vikundi  vya ushirika,  ili waweze kujipatia kipato cha halali.

Ushauri huo umetolewa na katibu wa kikundi cha ushirika  mapambano coperetive kinacho jishuhulisha na ufugaji wa Samaki, kaa, kamba  na mboga mboga  Bishara Muhammed Musa mbele ya  wanakikundi hao,  mara baada ya kuzungumza na mwandishi wa habari huko kikunduni kwao Sizini wilaya ya Micheweni Pemba.

Alisema wakati umefika  kwa vijana  kuwamka na kujiajiri wenyewe, na sio kukaa tu vigengeni na kusubiri ajira Serikalini.

‘’Vijana  mtakapo jiajiri mtaepukana na  vitendo vya wizi, ubakaji na ujambazi,’’ alishauri katibu.

Aidha  alieleza kuwa  sera ya Serikali  ya mapinduzi ya Zanzibar ya uchumi wa buluu  unaelekeza zaidi kwenye bahari, hivvyo  aliwasisitiza  viajana hao   kukiendeleza kikundi chao kwa juhudi zote, jambo ambalo litawawezesha kupata ursa mbali mbali za kimaendeleo.


 Mapema mwanakikundi Khadija  Ali  Juma alieleza kuwa ameamua kujiunga kwenye kikundi  cha ujasiriamali, ili aweze kujipatia kipato  kitakacho msaidia katika familia yake.

Aidha alisema mafanikio hayaji tu kama ndoto, hivyo ni vyema kuwa wavumilivu kupitia changamoto zinazowatokezea ili waweze kukiikisha mbele kikundi chao.

Akieleza  changamoto zinazowakwaza  kikundi  hapo  ni vitendea kazi, ikiwemo maberi  pamoja  mapauro.

Mwenyye kiti wa kikundi hicho Khalfan Hamad Khalfan alieleza kuwa  matarajio yao ni kuhakikisha wamekuwa wazalishaji wakubwa  wa mazao ya baharini.

‘’Tunatarajia kuzalisha  Tani moja  ya kaa, na  Tani moja ya Kamba  kila baada ya miezi miwili, na tani moja ya Samaki ndani ya kipindi cha mwaka mmoja,’’ alisema mwenyekiti.

Hivyo aliomba wizara ya uchumi wa buluu kujitokeza na kuwaunga mkono vikundi ambavyo vimewekeza juhudi zao kwenye maeneo ya bahari, ili waweze kunufaika na fursa zilizomo,  ndani ya  sera ya uchumi wa buluu.

Nae  afisa kutoka wizara ya uchumi wa buluu Pemba Mohd Ali  aliwapongeza Vijana hao kwa kuondosha dhana ya kusubiri ajira Serikali na kuamua kujiajiri wenyewe.

Aliendelea kusema Serikali haina uwezo wa kuajiri watu wote, hivyo ni vyema vijana kuiga mfano wa wenzao hao kwa kujiajiri ili waweze kujipatia kipato cha halali sambamba na kuondokana na Umaskini uliokithi.

 

MWISHO.

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO