RUSHWA MUHALI BADO NI GUMZO KWA KESI ZA UDHALILISHAJI
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Kuepo kwa rushwa muhali katika jamii bado ni changamoto
kubwa inayopelekea
kukwamisha kwa kesi za udhalilishaji
zisipate hatia.
Akitoa
ripoti juu ya kesi za udhalilishaji
mwendesha mashtaka wa serikali kutoka oisi ya mkurugenzi wa mashtaka Chake
chake Mussa Khamis katika kikao
cha kamati ya kupinga udhalilishaji kilichofanyika ofisi za Tamwa Kisiwani
Pemba.
Amesema
licha ya elimu inayotolewa kwa jamii ili kuacha muhali lakini bado hawaja kuwa
tayari juu ya mapambano dhidi ya udhalilishaji.
‘’Bila ya
mashirikiano ya pamoja hatuwezi tukafika pahala jamani tutabakia tunaimba tu kila siku alisema PP Mussa.
Aidha kwa
upande mwengine alifahamisha kuwa kesi zinazowapa changamoto katika uwendeshaji wake ni za
watoto wa miaka 15, 16 na 17 hawataki kutoa ushirikiano mahakamani.
Baadhi ya
wanakamati hiyo kutoka wilaya ya Mkoani wamekua wakivilalamikia vituo vya
Polisi Mtambile na kengeja kuwa bado havijakuwa makini kudhibiti vitendo ya
udhalilishaji.
‘’Sisi
tunashangaa kesi zinazoripotiwa vituoni humo watuhumiwa wengi wanakimbi
inakuwaje wasikamatwe’’ alisema Haji shoka kutoka mkoani.
Nae mratibu
wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa upande wa Pemba Fathiya
Mussa Said amewataka wanamtandao hao kuendelea kuchukua jitihada za makusudi
kuwaelimisha wanajamii kutoa tarifa mapema wakati unapotokezea udhalilishaji
samba mba na kuika mahakamani kutoa ushahidi.
Jumla ya
majalada 66 ya udhalilishaji yalipokelewa
katika ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP
mkoa wa kusini Pemba ambapo
majalada 37 yalifunguliwa
mahakamani, 21 yanaendelea na upelelezi na 8
yaliffungwa kutoakana na sababu za kiushahidi kwa kipindi cha Januari
hadi june mwaka huu.
Comments
Post a Comment