Kiungoni
walia na huduma ya Maji
NA
FATMA HAMAD, PEMBA
WANACHI
WA SHEHIA ya Kiuongoni wilaya ya Wete Kaskazini Pemba wamelalamikia juu ya kadhiya inayowakabili,
ya ukosefu wa huduma za Maji safi na
salama kijijini mwao.
Wananchi hao walisema tokea ulipoanza ujenzi wa barabara suala
la Maji ya Zawa vijijini mwao imekua ni kama ndoto, jambo linalopelekea
usumbufu wa kutafuta huduma hiyo maeneo ya mbali.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao, kiungoni mwananchi Zainab
Abdallah Hassan na Ngindo Kombo Faki walisema wanategemea huduma ya maji kupitia Kisima cha
Msikitini, ambapo kupandishwa kwake
kwenye Tenki ni nadra, kwani hadi wananchi walipie pesa ndio yapandiswhe.
‘’ Hayo maji
tunayotegemea hapo msikitini hayapatikani kama wananchi hawajachanga pesa,
hivyo kupatikana kwake ni shida,’ walisema.
Walisema kuwa tatizo hilo limeshakua kubwa na linahitaji
kuwangaliwa, kwani wakati mwengine wanashindwa kupata Maji hata ya kufanya
usafi majumbani mwao sambamba na kufulia nguo za watoto wao.
‘’Kwakweli tunashida kubwa watu wa kiungoni mana inabidi
tununue maji dumu shilingi miambili jee kweli hii ni hali tutaishi vipi sisi
majumbani na watoto,’’walisema.
Kwa upande wao Time Salim Hamad na Said Hamad Ali walisema kukosekana kwa maji kumeathiri
harakati za maendeleo ya wanakijiji wa Kiungoni, kwani wanashindwa kufanya
shughuli za kilimo na kuzalisha mazao ambayo yangeweza kuinua uchumi wao.
‘’Suala la kukosa huduma ya maji kijijini kwetu
limetuathiri, kwani tunashindwa kupanda hata mboga tukapata chakula kwani
hazikubali zinakufa kutokana na kukosa maji,’’walisema
Walisema mbali ya hilo pia wanaathirika kukosa maji ya zawa
kwani, wanawagonjwa pamoja na wenye ulemavu ambapo maji ya kununua ni tatizo,
wanashindwa kupata maji ya kutosha majumbani mwao.
‘’Tunawaomba
watendaji wa Mamlaka ya Maji itufanyie utaratibu juu ya suala hili, ukiangalia
sasahivi ni kipindi cha Ramadhani bila kuepo kwa huduma ya maji kijijini mwao
wanaathirika,’’walisema.
Sheha wa Kiuongoni Omar Khamis Othman alikiri kuepo kwa
tatizo hilo la huduma ya Maji kijijini humo.
‘’Ni ukweli uliowazi kwamba baada ya tu ya kuanza kwa ujenzi
wa barabara huduma ya Maji Safi ilikosekana kijijini hapo, na hii ni kutokana
na kukatwa kwa miundombinu ya mabomba yanayosambaza Maji katika maeneo
hayo,’’alisema.
Afisa mdhamini wizara ya Maji Nishati na Madini Injinia Suleiman Hamad Omar alisema
suala la kukosekana kwa huduma ya maji kijijini hapo limekuja baada ya
utengenezaji wa barabara.
Alisema ni vyema wananchi kuendelea kuwa na subra, kwani
ujenzi utakapomalizika na huduma itarejea kama awali bila ya shida yoyote.
MWISHO.

Comments
Post a Comment