AFUNGWA JELA MIAKA KUMI KWA UBAKAJI PEMBA


 


MAHAKAMA ya Mkoa Wete iliyopo Kaskazini Pemba imemhukumu kwenda chuo cha mafuno kwakipindi cha miaka kumi Khalfa Khalfan Mwaveso baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kubaka.

Mwaveso mwenye umri wa miaka 25 alitenda kosa hilo mwezi oktoba 2019, ambapo alimbaka msicha mwenye umri wa miaka 17.

Kabla ya kusomewa hukumu na hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamun, Mwaveso aliomba amahakama impunguzie adhabu ikiwa ni pamoja na kumpa kifungo cha nje ili aende kutumikia jamii.

“Naiomba mahakama yako inipunguzie adhabu ikiwa ni pamoja na kunipa adhabu mbadla ya kutumikia jamii kwani hili ni kosa langu la kwanza”alisema.

Hata hivyo upaande wa mashitaka ukingozwa na jopo la waendesha mashtaka Juma Mussa, Ali Amour na Mhammed Said waliiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia kama hiyo  kwani matendo ya aina hii yamekithiri ndaani ya jamii.

“Tunaiomba mahakama itoe dhabu kali kwa mtuhumiwa ili fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hii kwani matendo kama haya yamekithiri ndani ya jamii”alisema Juma Said.

Akisoma hukumu kwa mshitakiwa hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamuni alisema mahakama imeridhika na ushahidi ulitolewa na upande wa mashataka na hivyo kumuona kuwa ni mkosa ksheria na kumwamuru aende chuo cha  mafunzo kwa kipindi cha miaka kumi pamoja na kulipa fidia ya shilingi laki mbili kwa mwathirika.

Mratibu wa Chama Cha waandishi wa habari wanawake TAMWA ofisi ya Pemba Fat-hiya Mussa Said aliipongeza mahakama kutokana na maamuzi hayo.

Alisema TAMWA imepokea kwa furaha hukumu hiyo na kuziomba taasisi zinazosimamia sheria pamoja na wanajamii kushirikiana katika kuyatokomeza matendo hayo ndani ya jamii.

“Ikiwa kweli tunania ya kumsaidia Rais wa Zanzibar katika kuyatomeza matendo haya ya udhalilishaji kama ambavyo Mhe Rais ametangaza, ni budi kila mmoja kuhakikisha anashiriki kwa njia amoja ama nyengine kuwafichua wahusika wa matendo hayo”alishauri.

Katika kesi ya Mwaveso jumla aya mashahidi wanne walitoa ashahidi wao ambapo miongoni mwao ni daktari.


 





 

 


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.