Watendaji wa wizara ya maji kisiwani, Pemba wamelalamikia kunyimwa haki zao
Watendaji wa wizara ya maji kisiwani, Pemba wamelalamikia juu
ya ukosefu wa haki na fursa za kielimu
ambazo zimekua zikipatikana kupitia wizara hio kwa muda mrefu sasa.
Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya waziri wa wizara ya maji
na nishati Zanzibar Sleimani Masoud Makame,wakati alipokutana na watendaji wa
wizara hio kisiwani Pemba ambapo watendaji hao wamedai kua wamekua wakikoseshwa fursa
mbalimbali kutoka wizara hiyo ikiwemo fursa ya mafumzo.
‘’Mheshimiwa Waziri Mkurugenzi wetu mtu aliekua hana elimu ndio anaempa kipao mbele na maranyingi huwateuwa nafasi kubwa wale waliokua hawana elimu’’Walisema wafanyakazi wa wizara hiyo.
Baada ya kupokea malalamiko hayo waziri wa wizara hio
amemuagiza mkurugenzi wa mamlaka ya maji
Pemba Omari Mshindo Bakari, kushughulikia upatikanaji wa stahiki za wafanyakazi
hao.
‘’Mkurugenzi naomba kuanzia sasa kila mmoja hakikisha anapata
haki yake, sitaki kuletewa tena
malalamiko ya mtu kakosa haki yake’’Alisema Waziri.
Aidha waziri huyo amewataka wafanya kazi wa Mamlaka ya Maji
kutekeleza majukumu yao ipasavyo bila ya
ubaguzi, huku akiahidi kusimamia vyema haki za wafanya kazi hao .
‘’Acheni ubaguzi, acheni kufarakana, acheni kugawana naombeni mfanye kazi kwa mashirikiano’’Alisema waziri wa Suleiman.
Mbali na agizo hilo la kutaka kulipwa stahiki za wafanya kazi
hao, waziri amesema wizara yake
hatomvumilia mtendaji wa wizara hiyo atakaebainika anafanya ubadhirifu wa mali nakuahidi kuashughulikia watakao shindwa
kuajibika kazini.
Comments
Post a Comment