NA SAID ABRAHMAN
PEMBA.
WANAJAMII wametakiwa
kutunza mazingira yao na kuhifadhi maji taka ( maji machafu) ili kuepusha
maradhi ya mripuko yanayoweza kutokezea katika maeneo yao.
Hayo yalielezwa na
Bwana afya kutoka Baraza la Mji Wete Salim Mbarouk Rashid wakati alipokuwa
akizungumza na Mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Wete.
Alieleza kuwa
kumekuwepo na utiririkaji Mkubwa wa maji taka (machafu) katika majumba jambo
ambalo ni tatizo kubwa Kimazingira na hivyo kufanya mazingira kuwa katika
hatari na kuwa Kero katika jamii.
"Kutokana na Hali
ambayo ipo katika jamii,suala la kutiririka Kwa maji taka linahatarisha afya
Kwa wananchi na hivyo kupelekea kuibuka Kwa maradhi mbali mbali ya miripuko
ikiwemo matumbo na kipindupindu," alieleza Salum.
Aidha Salim
alifahamisha kuwa ikiwa Baraza la Mji Wete ndio wasimamizi wakuu wa Usafi
katika Mji wamekuwa na mikakati mbali mbali ili kuona hali hiyo inapungua au
kuondoka kabisa katika jamii.
"Mikakati ambayo
tumejipangia sisi Baraza la Mji Wete kuondosha hii kadhia ya kutiririka Kwa
maji taka kwanza ni kufanya ukaguzi wa mara Kwa mara katika majumba ili kuweza
kuwapa elimu Wana jamii jinsi ya kudhibiti maji hayo (maji machafu) kwani
imeonekana maji taka imekuwa ni tatizo kubwa katika jamii na Kwa Serikali Kwa
ujumla," alisema Afisa Salim.
Mbali na hayo lakini
pia Baraza limekuwa likihakikisha kuwa maji taka (maji machafu) yanadhibitiwa
Kwa kuwapatia elimu Wana jamii juu ya afya pamoja na kutunza mazingira.
"Sababu kubwa
ambayo inaonekana kutiririka Kwa maji taka (machafu) ni pale wanajamii
wanapoamua kujenga nyumba zao Huwa wanasahau kuchimba shimo la kuhifadhia maji
hayo na badalayake wao wanachimba shimo moja tu la kinyesi ilhali kunahitajika
mashimo mawili, kwani sheria ya mazingira ya mwaka 2011 na 2012 Namba 11
imeelekeza hivyo," alisema Salim.
Sambamba na hayo Afisa
huyo alieleza kuwa wamegunduwa Kwa wanajamii wengi hawaelewi umuhimu wa
utumiaji wa shimo la utumiaji wa maji taka na ndio maana Baraza likaweza
kuchukuwa dhima la kutoa taaluma Kwa wananchi wote.
Akizungumzia suala la
adhabu Kwa mwananchi ambae atapatikana na hatia ya kutiririsha maji machafu
katika nyumba yake, afisa huyo alisema kuwa Kwa upande wa Baraza ni faini ya
Tsh, 20000/- ambapo faini hiyo ni ya papo Kwa papo huku akitakiwa kuchimba
shimo Hilo mara moja.
"Kwa upande wa
adhabu, mwananchi ambae atapatikana na kosa hili ni faini ya Tsh, 20,000/ ya
papo Kwa papo na baadae kuchimba shimo na endapo hakufanya hivyo tunampeleka
Mahakamani na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miezi (6) na faini laki 3
(300,000/-) alisema Salim.
Mapema afisa huyo
alifahamisha kuwa kazi za kitengo Cha afya Baraza la Mji ni kuhakikisha
kinasimamia Usafi wa mazingira, kusimamia uondoshaji wa taka ngumu ambazo
zinazalishwa katika maeneo mbali mbali ya Mji wa Wete.
"Lakini pia
kitengo hichi kina dhima ya kusimamia suala la Usafi barabarani pamoja na
kuhakikisha mitaro yote iko katika hali ya Usafi," alieleza Salum.
Comments
Post a Comment