WASTAAFU WATARAJIWA WAFUNDWA
NA FATMA
HAMAD FAKI PEMBA.
Kaimu
mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka
mfuko wa hifadhi ya jamii ZSSF Khatib Iddi Khatib amewataka wafanyakazi
katika tasisi za umma kuwa na utaratibu wa kuamzisha miradi nbali mbali wanapokuwa
kazini ili iwasaidie mara watakapo
staafu.
Ushauri huo
ameutoa wakati akiwasilisha mada juu ya matayarisho ya kustaafu katika mkutano
wa mafunzo ya wastau watarajiwa
uliofanyika katika ukumbi wa ZSSF Tibirinzi Chake chake Pemba.
Amesema Kila
mtumishi wa umma kwa vile ameajiriwa ajuwe kama kuna siku ataondoka, hivyo ni
vyema kubuni mbinu mbadala ikiwemo kuweka miradi ambayo itawapatia kipato cha halali katika
maisha yao ya kustaafu kwao.
‘’hatuwezi
kudumu milele makazini tukubali kuwa ipo siku tutaondoka hivyo ni lazima tuweke vyanzo ambavyo vitakuja kutupatia
kipato Pencheni sio kama mshahara haitoshi kuendesha maisha yetu’’alikumbusha
kaimu mkurugenzi.
Akifungua
mafunzo hayo Ofisa mdhamini wizara ya Nchi Fedha na Mipango Abdul wahab Said
Abubakar amewataka watarajiwa hao kuwahimiza wafanya kazi wenzao kufanya kazi
kwa uadilifu na kwa uwangalifu ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi jambo
ambalo litawafanya waweze kupata haki zao stahiki kutoka Zssf.
Mapema
akitoa mada juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dk Rahila Salim Omar amesema watu wengi wanaposatafu hupata
maradhi mbali mbali ikiwemo kupooza hivyo
ni vyema Zssf kuwa na muendelezo wa kutoa mafunzo kwa watarajiwa wastafu ili
waweze kuondokana na hofu jambo ambalo litaepusha kupata shida kama hizo.
Baadhi ya watarajiwa hao wastaafu wameishari
Ofisi ya Zssf kuweka vituo vya Hospitali maalumu ambavyo vitatoa huduma kwa
wafanya kazi watakao staafu.
Nae mkuu wa
kitengo cha uhusiano na elimu Zssf Raya Hamdan Khamis amesema lengo la mafunzo
hayo kwa wastaafu watarajiwa ni kuwakumbusha juu ya kujitayarisha na wakati wao wa kustafu ili waweze
kukabiliana na hilo
Comments
Post a Comment