KIRARE AFUNGWA JELA
NA FATMA HAMAD PEMBA
Mahakama ya
mkoa C iliyopo Chake chake imemuhukumu kijana Khamis Abdala Khamis maarufu [Kirare]
mwenye umri wa miaka 20 mkaazi wa Kangani wilaya ya Mkoani Pemba kutumikia chuo cha
mafunzo kwa muda wa miaka 19 na fidia ya shilingi Milioni mbili[200,000] baada
ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutorosha na kulawiti mvulana wa miaka 10.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka [DPP] Ali Amour
Makame ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo makosa yote mawili
alioyafanya ni makubwa na kwa maelezo kutoka kwa daktari ni kwamba amesababisha
ulemavu kwa mhanga, hivyo naiomba mahakama yako itowe adhabu kali ambayo
itakuwa ni funzo kwake na wengine wanaotenda makosa hayo.
‘’Jamii
imekua ikisikitika sana kwa matendo haya ya kihalifu hivyo nivyema mahakama
yako ikampa adhabu kali kijana huyo’’ alidai Dpp Ali.
Hakimu wa
mahakama hiyo Muumin Ali Juma amemueleza
mtuhumiwa kwamba mahakama imekuona na hatia kwa makosa yote mawili la
kutorosha na kulawiti,hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 299 sheria nambari 7/2018
sheria ya Zanzibar kosa la kwanza utatumikia chuo na Mafunzo kwa muda wa miaka
5, ambapo kosa la pili la kulawiti kwa mujibu wa kifungu cha 7[a] sheria namba
7/2018 sheria ya Zanzibar utatumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 14.
Kabla, ya hukumu huyo, mshtakiwa Khamis
Abdalla Khamis ‘kirere’ miaka 20 wa Kangani wilaya ya Mkoani Pemba, alimtorosha
na kisha kumlawiti mtoto wa miaka 10.
Ambapo
alimtorosha kutoka sokoni Kangani na kumpeleka kwenye banda analolala, ambaapo
hilo ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (1) (b) cha sheria ya Adhabu sheria
namba 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Huku kosa la
pili alilotiwa hatiani ni la utawiti, wa mtoto huyo ambalo ni kosa kinyume na
kifungu cha 115 (1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya
Zanzibar.
Comments
Post a Comment